Bukobawadau

Mtu mfupi zaidi duniani...

Huko Philippines amegundulika mtu mfupi zaidi kuliko wote duniani, jamaa anaitwa Junrey Balawing anatoka katika kijiji cha Sindangan kusini mwa Ufilipino. Inadaiwa kuwa mshkaji ana urefu wa futi 2 tu ambapo siku ya tarehe 12.06.11 ametimiza miaka 18!

Kwamujibu wa msemaji wa kitabu cha matukio yanayovunja rekodi duniani cha Guinness amesema kuwa imechukuwa kitambo kuweza kumtambulisha rasmi jamaa huyo na kwa kawaida ili mtu apate kutambulishwa rasmi kama mvunja rekodi kwa nyanja hiyo lazima awe mtu mzima yaani afikishe miaka 18 ambayo tayari mjamma kesha ikwarua.

Balawing akiwa na wadogo zake.
Balawing hajaweza kukua tangu alipo sherehekea mwaka wake wa kwanza kuzaliwa, hawezi kutembea kawaida bali kwa kuhangaika na hawezi kusimama kwa muda mrefu, lakini pamoja na yote hayo anajivunia kuvunja rekodi hiyo kwani kabla ya kutangazwa kuwa mtu mfupi kuliko wote duniani, kijeba huyo alisema “If I were the smallest man in the world, it would be very cool.” akimaanisha kuwa itakuwa powa sana kama atatawazwa kuwa mtu mfupi kuliko wote ulimwenguni, historia ambayo tayari amekwisha itimiza. Kila la kheri Mr Balawing.
Next Post Previous Post
Bukobawadau