Bukobawadau

KASHAI YAMEWAKUTA,WAJUTA KUKUTANA NA BAKOBA!!!!!! WACHAPWA 2-1 Bakoba wasema mpira si uwanjani tu!!!!....!!

Nusu fainali ya kwanza ya michuano ya SELEWI CUP iliozikutanisha timu za Kashai na Bakoba imefanyika huku timu ya Bakoba ikiibuka kidume mbele ya mashabiki walio jitokeza kwa wingi uwanjani Kaitaba.

Timu ya kashai ndio ilikuwa ya kwanza kujipatia bao mnamo dakika ya 30 ya kipindi cha kwanza lililo fungwa na mchezaji Yasin Abubakari.
wakionyesha uwezo mkubwa na kuwamudu vyema wapinzani wao ,wachezaji wa Kashai walikuwa na morali mkubwa saana wakisaidiwa na kelele za mashabiki kama ilivyo kawaida yao kuonyesha ushirikiano.

Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko makubwa huku vijana wa Bakoba wakionyesha uchu mkubwa kwa kasi ya ajabu na pasi zenye kufika.Ndipo zahama ilipo wakuta Kashai Fc aka Banyaluganda ,mara tu walipo onyesha dalili za kutepeta na kupoteana uwanjani kana kwamba wamepewa maji yenye kilevi na akuwa mwingine bali ni mchezaji mwenye skills ya hali ya juu Mgwao Ramadhani Mgwao alipo wasawazishia watoto wa Bandarini maarufu kama mwanzo mwisho bao safi na murua mnamo dakika ya 72.kabla ya Shamte Odillo kutupia msumari wa mwisho zikiwa zimesalia dakika 9 Mpira kumalizika na kufanya kidedea kuendelezwa pande za Ernest,bigambo na Msese na kuifanya historia ichukue mkondo wake ya Kashai kuwa wadogo dhidi ya Bakoba.

Mwamko wa mpira Bukoba mjini ni mkubwa saana kama unavyo jionea wingi wa watu sehemu moja ya Jukwaa.
Wakati huo soka na mtanange vikiendelea.
Abdul Malick Sudi Tibabimale aka Kadunguda.Katibu wa wilaya wa BUFA akionyesha bashasha kwa kile kinacho endelea.
Mdau wa Soka Abul razack Majid Mtangazaji 88.5 Kasibante FM Radio akifatilia jambo kwa ukaribu zaidi
Kwa hali ilivyo waweza kufikiri ni simba na Yanga uwanjani kumbe ni hali ya mwamko wa mpira wa miguu iliopo kwa sasa mjini Bukoba.
Anaonekana hana wasiwasi wala shaka kabisa ni mkuu wa Hitfaki na mlezi wa Kashai FC.Ndg Peter Raphael Mgisha ,hapo akielekea changing room wakati wa mapumziko kutoa mawaidha kidogo wakati timu yake ikiwa mbele kwa bao moja kabla kibao akijawabadilikia na kujambangwa 2-1 mpaka mwisho wa mpambano na kufanya historia ya kufungwa na Bakoba kujirudia na katika hatua kama hii ya nusu fainali.
Namna hali ilivyokuwa uwanja wa kaitaba na bado kitimtimu kipo jumatatu hii wakati wa nusu fainali ya pili itakayo zikutanisha timu mama za Miembeni FC wenye kauli mbiu ya aina Majotooooo na mahasimu wake wakubwa Bilele-home boy maarufu kama wa hapa hapa!!!!na kama ilivyo ada bukoba wadau blogspot tutakunyetisha kila kile kitakacho jiri
Next Post Previous Post
Bukobawadau