Bukobawadau

MASHINDANO YA POOL TABLE YAFIKIA TAMATI.!!!Club bingwa yanyakua Tsh 700,000/=

Hiki ndicho kikosi kitakacho wakilisha mkoa wa Kagera kwenye mashindano ya kitaifa.
Pichani ni Msimamizi kitengo cha usalama ndani ya Q Bar akifatiwa na Mkurugenzi wake Ndg Samola Lyakurwa,katikati ni Mh Ibrahimu Idd Mabruki ambaye ni diwani wa kata bilele ambayo ndio kitovu cha mchezo huo wa pool unaoshika kasi saana kwa sasa na wa Mwisho ni Ndg Radislaus maarufu kama Kamisaa wa mchezo
Matumaini ya wao kupata ubingwa yanazidi kufifia kama unavyo waona.
Mchezaji wa timu ya Q bar Abdul-aziz akijaribu kufanya snook bila mafanikio yoyote.
Mzee Kagenda mdau mkubwa wa mchezo wa pool akionekana katika hali ya kustahajabu matokeo baada ya timu yake kupoteza ubingwa uliochukuliwa na timu ya sokoni maarufu kama (watoto wa mchungaji)
Anaonekana huyo dada akishangilia baada ya kutangazwa kama mshindi wa kwanza na pekee kwenye timu ya mkoa ya wanawake na amejipatia tiketi ya kushiriki mashindano ya kitaifa ya safari lagr pool tabbe yatakayofanyika kitaifa mkoani Dodoma
Next Post Previous Post
Bukobawadau