Bukobawadau

BAADAA YA MIAKA 50 YA UHURU KWA HALI HII TANZANIA TUTAFIKA.....BUKOBAWADAU TULITEMBELEA MAENEO YA BUKOBA VIJIJINI,KATA YA KIBIRIZI KIJIJI CHA AMANI NA KUJIONEA WANANCHI WANAVYOKABILIWA NA HALI NGUMU YA MAISHA.

Kivuko cha kyanyabasa kuelekea Ntoija,kishogo kata ya kashalu hadi Nyakibimbiri kuelekea kibirizi
kama unavyojionea katika picha hilo dimbwi la maji ambayo wananchi wa amani watumia katika matumizi ya nyumbani pamoja na mifugo
Mabwawa ya maji kama yalivyokutwa na Camera yetu,na hiyo ndio hali halisi ya upatikanaji mgumu wa maji katika kata ya Kibirizi/Bukoba vijijini ambapo wakazi takribani 6325 wanakabiliwa na uhaba wa maji katika kata nzima hawana kisima hata kimoja,Upatikanaji wa maji ni mpaka kipindi cha mvua,ambapo huchmbwa madimbwi katika miteremko ili yatunze maji,kama inavyoonekana katika picha maji hayo ndio hutumika kwa matumizi ya nyumbani na mifugo.
Katika kipindi cha Kiangazi wananchi wa maeneo hayo hulazimika kutembea urefu wa Km 16-32 katika eneo la Lake Ikimba au Rugaze Izimbya au katika Runch iliyoko Kibirizi.

Hiyo ndio hali halisi ya maeneo hayo ya Bukoba vijijini katika kata ya kibirizi watoto ndio wasombaji wakubwa wa maji kama walivyokutwa na kamera yetu,Je sisi kama watanzania tunalichukuliaje hili jambo?Wewe kama Mtanzania mwenye uchungu tunaomba utoe mawazo yako juu ya utatuzi wa tatizo hili kwani hali inasikitisha sana katika maeneo hayo.Nawasilisha hoja.Picha na Nambwegele Lukondo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau