Bukobawadau

BREAKING Newzzzzzzzzzz Kaitaba kwafukuta,Maji yashingo yamemkuta Ndg Malik apewa kichapo na raia!!!!!

Kiongozi wa Miembeni Fc Ndg Jamal Kalumna akimtupia shutuma kwa maneno makali na hisia kali katibu wa BUFA Wilaya ya Bukoba Mjini na msimamizi wa Kagasheki Cup Ndg Malik Tibabimale a.k.a (Kadunguda),sakata hilo limetokea md mchache baada ya kutokea sintofahamu kwa kile kilicho elezwa kwamba mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu kati ya Bilele na Miembeni umeailishwa na badala ya kuchezwa leo jumamosi basi timu hizo zitakutana kesho jumapili.

Kitendo cha kubadilisha ratiba hiyo kilipingwa vikali na uongozi wa Miembeni ndipo walipo chukua uwamuzi wa kupeleka timu yao uwanjani kwa misingi kwamba ratiba ya awali ilionyesha mchezo ni leo hii jumamosi ya tarehe 3-9-2011.

Sakata hilo liliweza kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka hususani wale wafatilia wa michuano hii ya Kombe la Kagasheki,na ikapelekea wadau wa soka kumtembezea kichapo Ndg Malik na kumlazimu kukimbia na kuomba hifadhi jirani kwenye mghahawa uliopo jirani na uwanja wa Kaitaba.
Bukobawadau tulikuwepo hapo kufatilia kila tukio kama utakavyo jionea katika picha.

wadau uwanjani kaitaba wakimzonga Ndg Malik
Wakati yote yakitokea Ndg Malik ameandaa mpambano wa wanawake na hapo ndio timu zikiwa zinasubiri kukaguliwa
Abdulrazak Majid Mtangazi wa 88.5 Kasibante Fm Radio akijaribu kuweka diplomasia juu ya labusha zilizo jitokeza uwanjani kaitaba
Mdau G Smart katika kustahajabu yaliopo mbele yake
Wanaonekana wachezaji wa Miembeni wakiwa hawana dira wala mwelekeo waliamua kuwa wapole kwani kwa mtiririko huu wa matukio,na kanuni hizi zinazofatwa kutokana na mazingira si ajabu mchezaji akapewa kadi nyekundi hata kama hakuna mchezo unao endelea.
Baada ya mshikemshike na taflani wadau na mashabiki wameonekana wakitoka nje ya uwanja huku kila moja akichukulia kitendo kwa mtazamo wa kipekee,na mda huu tayari Ndg Malik amesha kimbilia kwenye mghahawa uliopo kwenye vyumba vya uwanja wa kaitaba
Nje ya uwanja wa Kaitabu wadau wakimsubilia Malik baada ya kukimbia na kufungiwa kwenye chumba cha mghahawa hapo jirani
Next Post Previous Post
Bukobawadau