Bukobawadau

KASHAI WANYALUGANDA WATEPETA MBELE YA BAKOBA; mwanzo mwisho mabingwa Kagasheki Cup 2011

Pamoja na kutokuwepo na kiingilio uwanjani kuna wadau ambao raha yao ni kushuhudia wakiwa juu ya miti kama walivyokutwa na Camera yetu leo hii
Kikosi cha Bakoba kilicho chukua ubingwa wa Kombe la Kagasheki hii leo

Michuano hii leo imefikia tamati na Bakoba kuibuka kidedea kwa kuwafunga Kashai a.k.a banyaluganda 1-0.kikubwa ni umati mkubwa wa wadau unavyo guswa na michuano hii kama unavyo jionea
Mashabiki ni wengi uwanjani toka saa 7 mchana hali ilikuwa hivi
Mgeni wa heshima na mwakilishi wa Mdhamini wa ligi hii ni Ndg Abdul Kagasheki(katikati) ambaye pia ni Mwenyekiti wa wazazi CCM Mkoa wa Kagera
Anaonekana Ndg Amin Abdul akiteta jambo na mtangazaji wa mpra huu Abdulrazak Majid mtangaji wa 88.5 Kasimbante Fm Radio na mdau mkubwa wa libeneke hili la bukobawadau
Ramadhani Kambuga RMK na Erasmus George Kadanke Misifa
Viongozi mbalimbali wakiwa na wachezaji wa Bakoba na Kombe lao.
Mkusanyiko huu ni mashabiki wa Bakoba baada ya kipenga cha mwisho
Shabiki wa Kashai akiwa amejichora kichwani kwa kunyoa (inasomeka kashai Fc kichwani kwake)
Upande wa usalama hali ilikuwa shwari kutokana na udhibiti wa jeshi la Polisi

Next Post Previous Post
Bukobawadau