Bukobawadau

Mdau mwenzetu yamkuta ni Kijana wa Uswahilini Bilele

Wahenga walisema ‘za mwizi arobaini,’ ndivyo ilivyodhihirika kwa kijana mtanashati ambaye jina sitolitaja kwa sababu za kiusalama ila na mzaliwa wa hapa mjini bukoba na masikani yake ni uswahilini ndani ya kata Bilele (pichani)pale alipoonja machungu kufuatia kula kipondo kutoka kwa wananchi wenye hasira baada ya kudaiwa kuiba bidhaa kutoka kwenye Supermarket.

Tukio hilo la aibu lilijiri Septemba Mosi, 2011 ndani ya Supermarket ya TSN, iliyopo Bamaga- Mwenge, jijini Dar es Salam.
Mbali ya kipigo, wananchi hao walimsaula suruali kwa lengo la kumlawiti wakidai kuwa, itamfundisha na kuacha tabia ya wizi.
Baadhi ya watu nje ya supermarket hiyo walisema, jamaa kama alitaka kupeleka vitu hivyo kwa mkewe, basi ameonja machungu ya sikukuu, kwani alitakiwa kufanya kazi kihalali ili Eid iwe njema kwake.

Akisimulia ‘ei tu zedi’ ya tukio hilo, mfanyakazi mmoja wa supermarket hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema siku ya tukio, njemba hiyo iliingia dukani hapo saa 4 asubuhi na kusalimia kisha kuzunguka ndani akiangalia bidhaa kama ilivyo kwa wateja wengine.

Alisema kuwa, kwa jinsi alivyovaa kitanashati na tabasamu ambalo lilikuwa halimtoki mdomoni, hakudhani kama lengo lake lilikuwa kuiba.
“Alinikuta nimekaa na huyu mwenzangu, akatusalimia huku akionesha tabasamu la fedha, akaingia dukani na kuanza kuzunguka akiangalia bidhaa,” alisema mfanyakazi huyo.
Aliongeza kuwa, baada ya dakika kumi na tano, jamaa huyo alichomoza akiwa hana kifurushi chochote mkononi, lakini kiunoni alionekana kutuna na mwendo kubadilika, ndipo wakamtilia mashaka.

Alisema wakati akitoka mlangoni, mlinzi naye alipata wasiwasi dhidi yake na kumlazimisha kumsachi kiunoni na kukuta amechomeka mafuta ya kujipaka aina ya Nivea Body Lotion, Veseline, dawa ya meno ya Sensodyne pamoja na mafuta ya nywele ya Vitika, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 25,000.
Kijana huyo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar kwa mahojiano kisha kukimbizwa Hospitali ya Taifa, Muhimbili kunusuru uhai wake kwa vile hali yake ilikuwa mbaya kutokana na kipigo alichoshushiwa.

Next Post Previous Post
Bukobawadau