Bukobawadau

Mlimbwende anayejipatia malisho kwa njia ya filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, amefunua kinywa na kutema kauli tata…

Mlimbwende anayejipatia malisho kwa njia ya filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, amefunua kinywa na kutema kauli tata kuwa anapokuwa mbali na mpenzi wake Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’, kitu pekee kinachompa faraja ni pombe.

Akizungumza na The Biggest IQ Paper, jijini Dar juzi, Wema aliweka kweupe kuwa, anapokuwa mbali na laazizi wake huyo, njia pekee ambayo huitumia kuondoa mawazo na kukidhi hisia zake za kimapenzi ni ‘kujimwagia ulabu’ ambao humfanya ajihisi yuko na staa huyo wa Ngoma ya Moyo Wangu.

“Diamond amesafiri kwenda Uarabuni kutafuta maisha, unajua anaposafiri baadhi ya watu hudhani kuwa ‘nabanjuka’ na wanaume wengine, lakini ukweli ni kwamba huwa najiliwaza kwa pombe kali,”alisema
Wema.

Next Post Previous Post
Bukobawadau