Bukobawadau

Hii nayo Vipi tena?!!!!Mrembo Azeeka Ghafla Baada ya Kutumia Madawa ya Asili

Nguyen alivyokuwa mwanzo na jinsi alivyo sasa

Alikuwa ni mwanamke mrembo mwenye umri wa miaka 23 lakini baada ya kutumia madawa ya asili katika hali ambayo watu wengi walishindwa kuamini ndani ya siku chache alianza kuzeeka kwa kasi na hazikupita siku chache alionekana ni kama bibi wa miaka 73.
Miaka mitatu iliyopita, Nguyen Thi Phuong wa nchini Vietnam alikuwa na umri wa miaka 23, alikuwa ni mwanamke mrembo mwenye sura ya kuvutia lakini kutokana na tabia yake ya kutumia sana madawa ya asili, mwili wake ulizeeka ghafla ndani ya siku chache na ghafla alionekana kuwa na umbile na sura sawa na ya bibi mwenye umri wa miaka 73.

Nguyen alianza kuzeeka ghafla baada ya matumizi ya dawa za mitishamba na ndani ya siku chache tu aligeuka kuwa bibi wa miaka 73.

Nguyen Thi Phuong anaamini kuwa hali aliyonayo imesabishwa na aina ya samaki aliokula ambao waliusababishia mwili wake aleji iliyopelekea mwili kuwa katika hali aliyo nayo sasa.

Madaktari hata hivyo wanafikiri tofauti, wanaamini kuwa tabia ya Nguyen Thi Phuong kupenda sana dawa za mitishamba ndiyo iliyosababisha awe hivi baada ya mwili wake kupata aleji ya baadhi ya mitishamba.

Madaktari wanasema kuwa Nguyen anasumbuliwa na ugonjwa unaoitwa Lipodystrophy ambao husababisha kuyeyuka kwa kasi sana mafuta ya chini ya ngozi wakati ngozi yenyewe ikizeeka kwa kasi ya ajabu.

Ilielezwa zaidi kuwa mwili wa Nguyen ulikuwa na miwango kikubwa sana cha cortisol iliyotokana na mitishamba.

Hivi sasa Nguyen ana umri wa miaka 26 lakini anaonekana kama bibi wa miaka 76.

Nguyen anapewa sapoti kubwa sana na mumewe ambaye amedai kuwa pamoja na hali ya Nguyen bado anampenda kama siku ile aliyoanza kuwa na uhusiano naye.
Next Post Previous Post
Bukobawadau