Bukobawadau

IJUMAA YA LEO CAMERA YETU PANDE ZA BANDARINI:Bila shaka mdau unaikumbuka Meli ya Mv Victoria toka 1959-2011 na Bado inaendeleza historia!!!

katika pitapita zetu Bukoba wadau tumekumbana na Meli hii,Meli yenye historia kubwa sana kwenye manispaa yetu,wakazi wa mkoa wa kagera wamekuwa wakipata mahitaji ya kuingia na kutoka kupitia meli hii.

Ni Meli inayoitwa MV Victoria,kama inavyoeleweka moja ya njia za kuingia mkoani Kagera basi maji ni njia mojawapo,meli hii inayotoa huduma ya abiria na mizigo kwa gharama nafuu inaingia na kutoka mkoani Kagera kila siku ya jumatatu,jumatano na ijumaa

Ni meli ya siku nyingi sana,mpaka sasa bado ni tegemezi
Imesafirisha watu wengi sana katika historia'wananchi wengi
Wasomi wengi wanaikumbuka ambao leo ni maofisa wakubwa
Viongozi wengi ndani ya Nchi na nje wanaikumbuka kwa ujumla
kipindi wanasoma huku kagera,walitumia Meli hii kuja na kurudi makwao

Hapo inaonekana ikipakia Ndizi na mananasi kupeleka mikoa ya Mwanza na kwingineko,
Je Mdau unaikumbuka MV.Victoria?

Unanini cha kusema kuhusiana na Meli hii

Toa maoni yako kupitia google account yako

Au waweza kutoa maoni yako sehemu ya comment hapo chini

Waweza pia kusema lolote na chochote kupitia facebook page yetu

Au mwisho kabisa wa page hii kuna sehemu ya maoni kupitia facebook

Bukobawadau tunazidi kuwashkuru wadau wote wanaotupa ushirikiani

Next Post Previous Post
Bukobawadau