Bukobawadau

MATUKIO YA SWALA YA IDD ADHUHIA;Swala imeswaliwa msikiti wa Ijumaa,imeongozwa na Imamu Yusuph Issa ambaye ni imamu wa msikiti wa Ijumaa manispaa ya Bukoba na kufatiwa na baraza la Idd katika msikiti huo huo baada ya swalat aswil lililo ongozwa na Sheikh wa Wilaya ya Bukoba Mjini Sheikh Haruna Abdallah Kichwabuta...

Pichani Haji Hamza Omary kiongozi wa msikiti wa Ijumaa akimkaribisha mwenyekiti wa baraza kuu la Waislam wa Tanzania (Bakwata) mkoa Al haji Abubakari Sued Kagasheki.
Al haji Abubakari Sued Kagasheki Mwenyekiti wa Mkoa wa Baraza kuu la waislam wa Tanzania Bakwata.
Wadau Waumini Wakimsikiliza khutuba ya Idd kwa Umakini.
Anaonekana muhandisi wa Maji wa Wilaya Al haji Ahmada Kantunsimbi ambaye ni miongoni mwa wahumini walio hudhulia Ibada ya Idd
Sheikh wa Wilaya ya Bukoba Manispaa,Sheikh Haruna Kichwabuta akisoma hutuba ya Idd Adhuhia ilioswaliwa Msikiti wa Ijumaa Bukoba Mjini.

Pamoja na mambo mengine sheikh alichukua fursa hiyo kumlaani vibaya Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon kwa kitendo chake cha kisheitwani alicho kitenda hivi karibuni kwa kutangaza kuwa Uingereza haitasaidia nchi yoyote isiokubaliana na Ushoga

Aidha Sheikh Haruna aliongeza kwa kusema kuwa kitendo cha Waziri huy kimewadhalilisha Waingereza wote hususani Dhehebu zima la Anglican kote Duniani

Mwisho aliwasihi Waislam wote kuwa tayari kupigana kufa na kupona pale tu itakapodhihilika katika jamii yetu uwepo wa kukubaliana na vitendo hivyo haramu vilivyosababisha Mwenyezimungu S.W kuangamiza kaumu(umma) nzima ya watu wa Nabii Lutu walipojiingiza katika uchafu huo maarufu kama Sodoma na gomola.

Al haji Ayub Ali Kagire Mwenyekiti wa Baraza la Waislam Bakwata Bukoba Mjini naye akimsikiliza kwa makini Sheikh Haruna Kichwabuta.
Sheikh Ismail Jaffar muhakiki mahesabu wa Msikiti wa Ijumaa Bukoba Mjini akihakiki fedha iliopatikana katika swala ya Idd kwa ajili ya Madarasat Fauz.
Pichani sheikh Haruna anaonekana kumsikiliza kwa umakini mkubwa m/kiti wa elimu mashuleni ustadh Twalibu Temani wakati alipowatunukia zawadi washindi walioongoza kwenye mtihani wa maarifa ya dini ya kiisilamu darasa la saba uliofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania nzima na mkoa kagera kushika nafasi ya kwanza kitaifa.
Ustadhi Twalib Temani Mwenyekiti wa Elimu mashuleni.
Mwanafunzi akipokea Zawadi kutoka kwa Mgeni Rasmi Al Haji Abubakari Sued Kagasheki.
Next Post Previous Post
Bukobawadau