Bukobawadau

MKUTANO WA KIHISTORIA KATI YA RAIS KIKWETE NA UONGOZI WA CHADEMA IKULU DAR ES SALAAM NOVEMBA 27, 2011

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza maelezo toka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe baada ya kupokea mapendekezo ya chama hicho juu ya kuundwa katiba mpya yatayozungumzwa kwenye mkutano huo wa kihistoria uliofanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa CHADEMA katika mkutano huo wa kihistoria
Mkutano ukiendelea
Rais Jakaya Kikwete akiongea na uongozi wa CHADEMA (kushoto) pamoja na ujumbe wa Serikali (kulia)
Mh. Tundu Lissu akikoroga chai baada ya mkutano huku Profesa Baregu naye akijiandaa kujisevia
Rais Jakaya Kikwete akimpa juisi Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe baada ya mkutano
Rais Kikwete na wageni wake wakilegeza makoo baada ya masaa mawili na nusu ya mkutano
Furaha ilitawala baada ya kumalizika kwa mkutano na wageni kuinuka na kuaga
”….Asante sana Mh Rais kwa kukubali mwaliko wetu…” anasema Mh Freeman Mbowe wakati akiaga
Profesa Mwesiga Baregu akiaga
Profesa Abdallah Safari akiaga
Kwaheri Mheshimiwa na asante kwa kutukaribisha Ikulu…
Kaimu Katibu Mkuu Mh John Mnyika akiaga. Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa alitoa udhuru kuwa unauguliwa hivyo hakuweza kufika
Mh Tundu Lissu akiaga
Mh Tundu Lissu akiondola Ikulu taratibu baada ya mkutano huku gari iliyombeba mwenyekiti wa CHADEMA ikiondoka pia…...

CHANZO:kurugenzi ya Mawasiliano ya Ofisi ya Rais-Ikulu
Next Post Previous Post
Bukobawadau