Bukobawadau

MDAU NOELA OWONYESIGA ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA NTOMA-MARUKU NA KUTOA ZAWADI MBALIMBALI NA CHAKULA

Anaonekana mdau Noela kushoto na Mdogo wake Nicolas Ishebakaki mara tu walipo kitembelea kituo cha watoto yatima kituo hiki kipo Ntoma- Maruku wilaya ya Bukoba vijijini

NDG WADAU KILA mmoja wetu atakubaliana nami kuwa maisha tunayoishi siku hadi siku yametofautiana kwa kiasi kikubwa sana, kuanzia mtu mmoja, jamii hata taifa kwa taifa.

Hali hiyo sasa inatufanya tuwe katika makundi mbalimbali katika jamii, hivyo basi katika hili kuna kundi ambalo linajiweza na halitegemei kusaidiwa na lingine linahitaji msaada wa vitu muhimu katika maisha.

Msaada mkubwa wa kwanza katika kundi lisilojiweza ni chakula ndipo mengine yafuate, lakini moja kwa moja tunatambua kuwa watoto yatima waliokosa walezi na watoto waishio katika mazingira hatarishi ndio walengwa wakubwa katika kundi hili

Akiongea na Bukobawadau Bi Noela Owonyesiga amesema;'anaomba watu tuwasaidi,tuwatie moyo,tuwapende na mengine yote tutalipwa na Mungu
Mdau Noela akiwa na mtoto wa miezi 6 aliyeletwa kituoni hapo siku ya pili baada ya kuzaliwa na mama yake kupatwa na mauti.
Wanaonekana watoto ambao kidogo wameanza kukuwa kwa kulinganisha na umri wa siku moja au mbili wanapofikishwa hapa kituoni.
Bukobawadau blogspot tunaiasa jamii kujitolea misaada mbalimbali kuwasaidia yatima
Chakula na zawadi mbalimbali vilivyo tolewa na Mdau Noela.
Bi Noela katika hali ya mshangao kwa kile anacho elezwa na Mlezi.
Mama Mlezi Bi Evelyn akimwonyesha Mdau Noel mtoto aliye pokelewa akiwa na uzito wa kilo 1.7 na kwa sasa anaendelea na afya nzuri.
Bukobawadau tunaomba kwa yoyote mwenye uwezo au Chochote aweze kutembelea kituo hiki kwani msaada zaidi unatakiwa kwa wadogo zetu mayatima kwani watoto ndio taifa la kesho(na ni vyema ukaifanya hii kama furaha yako ya kuumaliza mwaka na kuukaribisha mwaka mpya)..

Naonekana blogger Mc baraka nikiwa katika hali ya udadisi zaidi kwa kumtazama mtoto Alicea mwenye umri wa mwezi mmoja amezaliwa tarehe 19-12-2011 na Mama yake akakutwa na mauti siku hiyo na kututangulia mbele ya haki.
Pamoja na kile kidogo nilicho kitoa Mie Mc nimeweza pia kufanya mahojiano na Bi Evelyn Kamazima ambaye ndiye mhusika na mlezi mkuu hapa kituoni toka mwaka 1968.

Bi Evelyn amesema zipo changamoto nyingi zinazo mkabili moja wapo ikiwa ni swala la wazazi akina Baba kukataa kuwafata watoto wao pindi wanapofikisha umri wa kuwachukua makwao kwani utaratibu ni kwamba mtoto anapofikisha umri wa miezi 16 inabidi akabidhiwe kwa Mzazi wake au jamaa zake.

Aidha Bi Evelyn amesema anasikitishwa sana na tabia za watu wanao shindwa ata kuja kuwatembelea watoto wao na katika hili akakumbuka kisa cha mkazi mmoja wa Bugabo jina linahifadhiwa aliyefiwa na mke wake wakati anajifungua na kumwacha mtoto ambaye aliletwa kituani hapa ila miezi minne badae ikasikika huyo Baba ameoa mke mwingine na hakutaka tena kusikia habari za mtoto wake.
Hii hali inatisha wadau na inasikitisha sana.

Bukobawadau tukajikita zaidi katika kutaka kufahamu kituo hiki kina muda gani na yeye mwenyewe ameanza lini kuhudumia hapa na zaidi anapokea watoto wengi kutokea maeneo gani katika mkoa huu au Tanzania kwa ujumla na kituo hiki kinauwezo wa kuhudumia watoto wangapi?

Bi Evelyn akasema kituo hiki kilianza mwaka 1952 wakati huo yeye akiwa mdogo sana na baada ya masomo yake alianza kuhudumia mwaka 1968 na akatuonyesha kijana wake wa kwanza kumlea ambaye kwa sasa ni mtu mzima na anawatoto 6.

Ndg Joel Tibabileba pichani ndiye mtoto wa kwanza kupata malezi mikononi mwa Bi Evelyn,Ndg Joel mpaka leo anafanya kazi mbalimbali kituoni hapa na amebahatika kuoa na kwa sasa anafamilia yenye watoto 6
Mdau Joel picha ya pamoja na Mlezi wake Bi Evelyn na mlezi.
Mlezi wa kituo hiki cha Ntoma-Maruku akimshukuru na kumuaga Bi Noela
Mdau Noela akiondoka kwenye mazingira ya kituo hiki.
Mwonekano wa mazingira ya kituo hiki.

Bukobawadau tunawaasa wadau kutoa chochote kwa watoto yatima.
Bukobawadau tunawatakia Mayatima wote heri ya Mwaka Mpya.
Next Post Previous Post
Bukobawadau