Bukobawadau

JE UNALIKUMBUKA GUMZO HILI 2011 ?!Bukobawadau blogspot katika kumbukumbu by Mc Baraka.

Kama kuna tukio hatuwezi kulisahau kwa mwaka uliokwisha wa 2011 basi ni mashindano makubwa kabisa kwenye Wilaya ya Bukoba Mjini,mashindano yanayobeba hisia kubwa miongoni mwa wakazi wa Mkoa wa Kagera na mikoa ya jirani na Nchi za jirani,haya sio mashindano mengine bali ni KAGASHEKI CUP Kipindi cha mashindano hayo,kama ungekuta kuna kikundi cha zaidi ya watu watatu kinajadili basi ujue kilikuwa kinaongelea mashindano hayo,kulikuwa na Fitna za kila namna kuanzia kwenye kusajili wachezaji mpaka mwisho wa mashindano
Ninakumbuka kiongozi mmoja wa kata Miembeni alivyofanikiwa kuwanyakuwa wachezaji tegemezi wa kata kashai bila viongozi wa kashai kuamini kilichotokea,Nakumbuka kata Miembeni pia walivyoweza kumnyakuwa kipa namba moja wa kata Bilele na kumtumia kwenye mashindani haya na wakiwaacha kata Bilele wakibaki kinywa wazi,nakumbuka libeneke la kiongozi mmoja wa chama cha Soka kwa kuleta sintofahamu kwa kushikilia sheria tata za Soka.
Ninakumbuka Kata ya bilele walivyofanikiwa kuunda kikosi imara chenye wachezaji wenye uwezo mkubwa na molari kubwa ya kupambana kweli kweli,Ninakumbuka kata Kitendaguro "makilikili" walivyoweza kuunda kikosi imara kilichowatoa jasho vigogo mbali mbali wa kata za mjini Ninakumbuka Fitna ya kata Rwamishenye wakiongozwa na Sued Kagasheki walivyounda kikosi cha ushindani na kuzipa tabu kata nyingine kwa soka yao ya hali ya juu,Ninakumbuka Fitna ya kata ya Hamugembe ikiongoza na kina Muganyizi na kina Pidi walivyoweza kusuka kikosi Imara kilichowakosesha timu pinzani usingizi na kufanikia kuichapa kata fulani kichapo kitakatifu Nakumbuka kata Buhembe walivyo mkaba koo mtu mzima na kufanikiwa kumchapa bao moja kwa bila,nazikumbuka kata Nyanga,kahororo,nshambya,ijuganyundo,kibeta,......
Shabiki wa Kashai akiwa hana la kusema baada ya kupoteza mbele ya Bakoba.
Hakika habari ikasomeka kama hivi'BAKOBA MWANZO MWISHO'
Wanayo kila sababu ya kushangilia kwa nguvu zote,mashujaa hawa wa soka wachezaji wa Kata bingwa kata Bakoba,hapo walipokuwa kwenye sherehe yao Ndani ya ukumbi wa linaz wakiruka goma la Mh.Temba na wanaume linalosema MKONO MMOJA WEKA JUU.....aaaah aaaah
Mapacha wawili wa kata Bingwa,Bakoba Mwanzo mwisho Salmin Athuman 'Babdinyo' ukipenda Iniesta na Ramadhan mgwao 'striker force' .Vijana hawa ilikuwa ni chachu ya magoli kwa timu yao. LIBENEKE LA BUKOBAWADAU BLOGSPOT KATIKA KUMBUKUMBU BY MC BARAKA.
Next Post Previous Post
Bukobawadau