Bukobawadau

Swala la Usafi wa Mazingira Bukoba linaendelea vizuri sana Ila Wenzetu Mjini Kampala hapanaaaaa!!!!

Hii ni hali ya Mtalo Mjini Kampala Katikati ya Mji Kuingia Nakivubo.
Hii ni Barabara ya Kiseka Mjini Kampala hali ni tete..Na hapa Ndio naungana na Mkuu wetu wa Mkoa wa Kagera Mh.Kanal Massawe kwa kulivalia njuga swala zima la usafi tena mtaa kwa mtaa,nyumba hadi nyumba,chumba kwa chumba.

Hapa Manispaa ya Bukoba hali si mbaya sana jitiada zinaonekana kabisa
.

Mwonekano wa Viunga vya Mji wa Bukoba Mchana huu wa Jumatatu 16-1-2012.

Nikiwa Stendi ya Mabasi najaribu pia Kuangaza kinachoendelea pembezoni ukanda wa kijani(green belt) upande wa Kibeta,Kitendaguro,Busimbe na Kashura ujenzi wa nyumba za wadau unaendelea kwa kasi.
Ukiwa Maeneo haya nilio yataja unaweza kuliona Ziwa Victoria kama hivi hii ni Bukobawadau blogspot katika kukuweka wewe mdau karibu na nyumbani au kujua hili na lile japo kwa mkutasari
Zafanana bus service
Hili Bus binafsi nimepanda sana kipindi Mji wetu una mabus matatu au manne ni maarufu kama "ZAFANANA" au Double Action mali ya Mzee Robozi wa Kibeta-Ibula
Nimependa huu msema nimevutiwa na hili Bus ni OTALIGAMBA luxury Coach.
Wadau wa Nshamba waleeee!!!!!
Nakutana na Mdau Denice Sheshema wa Kibeta ni mdau wangu sana, Kidato kimoja kwa walio somo Mugeza kipindi chetu mnamkumbuka.
Mchakato wa fulsa ya uwekezaji Nyumbani kasi inaendelea kama unavyo jionea Ndg Msomaji.
Ni moja kati ya Project zinazo simamiwa na Ndg Soter.A.Rwebangira wa Mutembei Holding CO.
Mwekezaji ni Mdau Ndg Thadeo Mutasingwa Mutembei
Bukobawadau tunatoa pongezi kwa kazi inayo endelea kwako Ndg Mutembei.
Next Post Previous Post
Bukobawadau