Bukobawadau

HAPA NA PALE NA CAMERA YETU;Mdau Al-Amin na Vijana Wenzake wasema 'Wameamua Kujisahihisha'Lowassa ni Jembe lao !!!!


Libeneke la bukobawadau limeanza kushuhudia baadhi ya vijana mjini hapa , asa wapenzi wa siasa wakitumia muda mwingi  kujadili watu na propaganda za kisiasa

 Kwa siku ya leo nimekutana na Kijana Maarufu Mjini hapa na maeneo ya jirani ajulikanae kwa jina la Al-Amin Abdul maarufu kama Amin Mnyee akiwa  na kundi la vijana na wazee jumla wapatao sita wakijaribu kuongelea hili na lile juu ya kwa nini wanamkubali  Mbunge wa Monduli Mh.Edward Ngoyai Lowassa 

Wamesikika wakisema kwamba, taifa linakabiliwa na changamoto nyingi kama zile za kuhamasisha uwezekazji wa ndani na nje ya nchi, kuimarisha mifumo ya utawala bora, kuporomka kwa thamani ya shilingi kila kukicha, mdororo wa uchumi, tatizo kubwa la ajira kwa vijana, kushuka kwa kiwango cha elimu na ugumu wa maisha kwa ujumla. TUNAPASWA KUJISAHIHISHA.


Akiongea na Bukobawadau mara tu baada ya kumuuliza kulikoni? Ndg Al-Amin  amesema maneno haya; Lowassa ni Jembe langu, namkubali kwa sababu yeye ndo kiongozi anayetakiwa kwa kipindi hiki na kuitoa nchi ilipo kwani ana utashi na ana uhakika na anachokifanya, hayumbishwi na mtu.

Bukobawadaublog sio wanasiasa ila tunapenda   maendeleo na ukweli !!!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau