Bukobawadau

ONYESHO LA ORIGINAL COMEDY MAMIA WAFURIKA UWANJA WA KAITABA




Mamia ya Watu walijitokeza kushuhudia Onyesho Maalumu linalofanywa na Wasanii wa  Orginal Comedy la kuchangia Ujenzi wa kanisa la  Evangelist Assemblies of God,lililopo Airport Nyamkazi Bukoba
Msanii MACREGAN   ukipenda unaweza kumuita Kipara aka (Shemeejiii) au mzee wa tuendeleeeeee akifanya mambo yake jukwaani.
 Ukipenda unaweza kumuita Bebari la Kihaya jina halisi ni Mjuni Silvesta maarufu kama Mpoki wa Orginal Comedy akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera kufungua rasmi  alambee ya Ujenzi wa Kanisa
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Massawe(kushoto) akifunguka juu ya kile anacho kitoa na kuashilia ufunguzi rasmi wa zoezi zima la uchangiaji wa Kanisa,Yeye binafsi ametoa kiasi cha sh laki tano(500,000)na Ofisi  ya Mkoa imetoa sh laki tano.
Msanii Masanja Mkandamizaji akiendeleza libeneke la alambee.
Mdau Peter Matagi akiwa hana mbavu na swaggar za Msanii Masanja Mkandamizaji.
Mdau pichani ni  Jeanifer Murungi Kichwabuta
Andunje aka  Joti in Action.
Pozy la Msanii Wakuvanga aka Baba Andunje (kulia)ama kwa hakika jamaa hawa wapo vizuri katika hii fani.
Msanii Joti aka Andunje namna anavyo kubalika.
Bila shaka Mdau utakubaliana na mimi kuwa msanii Joti  yupo katika chati ya juu kabisa kutokana na umahili wake wa kucheza nafasi mbalimbali katika vichekesho.
Mpoki Bepari La Kihaya - mwarabu wa dubai (Rick Ross wa sasa)Kushoto,hapa kikubwa ni cha chini alichotupia msanii Macregan (kulia)
Mh.Kamote Mkuu wa Wilaya kushoto na Mh. Anatory Aman Meya wa Manispaa ya Bukoba wakifatilia Onyesho kwa ukaribu.
Wasanii  wa kundi zima la Orginal Comedy kutoka kushoto ni Wakuvanga,Mpoki, Masanja, Joti na  Macregan
Kulia ni Ndg Balle Joseph  akipewa shavu na Masanja ya kwamba anafaa kuwa msanii.
MMMMMH!!!!!

Libeneke hili litaendelea Kesho usiku kwenye Ukumbi wa Linas Night Club.
Mamia ya Wadau waliojitokeza... hapo ni Baba ,Mama, Watoto hadi mkwe wakiangalia .


Wasanii Wakuvanga na Masanja wakiwajibika.

Onyesho hili ni maalumu kwa ajili ya alambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa la (EAGT)lililopo Nyamkazi Bukoba.
Next Post Previous Post
Bukobawadau