Bukobawadau

Whitney Houston Elizabeth (9 Agosti 1963 - 11 Februari 2012)

  Whitney Houston Elizabeth Mwanamuziki mashuhuri wa Marekani  amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48. 
(9 Agosti 1963 - 11 Februari 2012) alikuwa mwimbaji, mwigizaji, mtayarishaji.
Amefikia mafanikio makubwa sana mfano. Mwaka 2009, Guinness World Records alitangazwa kama mwanamuziki bora wa kike  kutokana na tuzo nyingi alizo  jipatia kwa wakati wote. 
 
Nimegundua Whitney Houston alikuwa na mashabiki wengi sana duniani kote na hii leo  nimepokea simu nyingi  kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwa na lengo la kunijulisha juu ya kifo cha Mwanamuziki huyu na wengine wakionyesha simanzi na majonzi makubwa  juu ya kifo chaWhitney.

 Mpaka nafanya Jitiada hizi  mie Mc  Baraka sijapata Sababu za kifo chake na mahala alipofariki bado hazifahamiki,

 Whitney Houston ni  msanii  wa kuchukua mfululizo 
No 1 Billboard Hot 100 hits hapo tunaongelea wimbo wa mapenzi yangu yote ni kwa ajili yako yaani My Love  is your love  "I Wanna Dance na Somebody Loves Me (mtu flani ananipenda) ,Nyimbo kama Emotional na nyingine nyingi.

Na kama nikibahatika kufanya enterview na wasanii wengi wa kike wa  Tanzania na East Afrika kiujumla  utawasikia wakisema wanampenda na wanafata nyayo za Whitney  hapo namaanisha Juliana Kanyamozi, JayDee, Aman ,Linnah na wengine wengi ,

Whitney Houston  mwaka  2010 alikuwa mmoja kati yawasanii wanao ongoza kwa mauzo dunia zaidi ya copy 170 milioni zimeuzwa duniani kote ikiwa ni single mbalimbali ,Album na Video. 
 , 

 Whitney HoustonHouston alianza kuimba na New Jersey  katika kanisa la injili  kama mwana kwaya akiwa na umri wa  miaka 11.  
Na  badae alijiunga na  mama yake na kuanza kuimba pamoja  katika klabu ya usiku katika eneo la New York City, ndipo alipo pata kujiunga  na Arista Records studio ya mtu mmoja mtata sana ajulikanae kama Clive Davis
   
Mpaka hivi sasa kazi za Whitney ni sawa na Almasi au Dhahabu ikiwa ni movie alizo cheza,nyimbo zake zote katika album mbalimbali na  soundtrack kama tatu zilizotumika.

Bobby Brown na Whtitney Houston

Whitney  kama mmoja wa wanamuziki wenye mafanikio makubwa duniani, na mcheza filamu mbalimbali vile The Bodyguard na Waiting to Exhale.
Fani yake iliwahi kuzongwa na matumizi ya dawa za kulevya na maisha yake yenye matatizo katika ndoa na msanii Bobby Brown kitu kinacho pelekea mpaka hivi sasa wadau wengi wamtazame Bobby  Brown kwa jicho la pili nikiwa na maanisha kutia shaka juu ya kuchangia katika mabadiliko ya Maisha ya Whitney.
 Bobby Brown  aliwahi kusema katika kitabu chake  namnukuu;“I never used cocaine until after I met Whitney. Before then, I had experimented with other drugs, but marijuana was my drug of choice,” Brown writes in “Bobby Brown: The Truth, the Whole Truth and Nothing But,” out next month. “At one point in my life, I used drugs uncontrollably. I was using everything I could get my hands on, from cocaine to heroin, weed and cooked cocaine.”


Next Post Previous Post
Bukobawadau