DR.YUSUPH M.KAMBUGA NA NURIAT HABIBU WAMEREMETA!!!!!!!!!!
Msafala baada ya kuwasili mjini kamachumu,Na katika hili bukobawadau tunakumbuka ni harusi ya pili ya Familia ya Kambuga mwenyeji na mzaliwa wa Bugabo anafanikiwa kupata Wakwe Kamachumu eneo la "wahamba"
Hii yote ni kuhakikisha kwamba Dr kambuga anapata mwenza,msafara wa magari ukiingia kamachumu maeneo ya mirama
Mdau yunusu Kambuga, Mdau wa Muleba Magatta jirani na kishoju katikati ni Mangi said na kulia ni Ndg Ramadhani Kambuga.
akina mama in ACTION katika hili namkumbuka mzee "Muyaga" kutokana n sifa kubwa ya ulimaji na utengenezaji wa mashamba mazuri ya Ndizi
Akina baba nao in ACTION
Wapambe wa bwana harusi upande wa akina mama
Kutoka kulia ni Mzee Maulidi Kambuga akiwa na wanae katikati ni mmiliki wa kampuni ya RMK ndugu Ramadhani Kambuga na Dr.Yusuph kambuga bwana harusi.
Sehemu ya wageni waalikwa upande wa wanaume wa pili kulia ni mzee Hemed Kiwanuka mmoja wa Mabalozi wa serikali ya hawamu ya tatu.
Bwana Gilbert George,nyuma kabisa ni Yunusu Kambuga akiteta jambo na Ndugu Sadick Top in Town.
Bwana harusi Dr.Yusuphu Kambuga akiwa katika uso wa bashasha.
Bi harusi Nuriati Habibu
Shahidi wa Bwana harusi akiweka sahihi kwenye cheti cha ndoa na kama ilivyo kawaida kama kuna mtu au mdau anae jitoac sana kwenye shughuli za watu akika kwa ukanda huu ni Mzee wetu Haji Jaffary(katikati)
Hapa ni kamachumu AL HALABA na Al- Saqry ndio tanulu.
Dr.Yusuph Kambuga akiwa na mkewe Nuriat Habibu kwenye gari tayari kwa safari ya kurudi nyumbani Bukoba.
Ndg wadau tungependa ushirikiano katika kupeana comment ili tupate na sie kufarijika na kujua ni habari zipi mngependelea kwani tunaamini yapo mambo ya kusifia na kukosolewa hilo ndilo la msingi kwetu
(Maharusi wetu hili jicho au macho haya sijui wadau wanasemaje........tuelezane...?)
Umependeza sana Bi Harusi
Maharusi wakiondoka kwa mbwembwe za kutosha,na hapa ni eneo maharufu sana ndani ya kamachumu wadau wengi wa ukanda wa Mulela, Kalela, Kishanda,Nshamba,Rubale na kiyanja yote mnakumbuka Jengo hili (kulia)ni hotel ya 'Mzee Kanyangalama' hotel yenye historia ndefu sana sambamba na mapishi mazuri BUKOBAWADAU TUNAKUMBUSHIA!!!!
BUKOBAWADAU TUNAWATAKIA MAHARUSI HAWA MAISHA MEMA NA YENYE BARAKA TELE