IJUWE HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA VIJIJINI ;Halmashauri yenye historia kabla ya Uhuru wa Nchi yetu!!
Mwonekano wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini(Chember)lililopo Mjini Bukoba.
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ni moja kati ya Halmashauri za Wilaya
nane zilizomo katika Mkoa wa Kagera. Halmashauri ya Wilaya hii ni
miongoni mwa Halmashauri kongwe nchini kwani imekuwepo tangu kabla ya
Uhuru wa Nchi yetu. .
Jengo hili limejengwa kabla ya Uhuru na jiwe la msingi limewekwa 4/11/1958 na Senior Proviancial Commissioner Ndg S.A. Walden.
Kijiografia Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ina jumla ya eneo lipatalo hekta
284,100, kati ya hizo hekta 2,293 ni eneo linalofaa kwa kilimo hekta 660
ni eneo la malisho ya mifugo, hekta 300 zimefunikwa na maji.
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba upande wa mashariki inapakana na Ziwa
Victoria na Halmashauri ya Manispaa Bukoba, kaskazini inapakana na
Wilaya ya Missenyi, magharibi inapakana na Wilaya Karagwe na kusini
inapakana na Wilaya ya Muleba.
Wilaya ipo katika vipimo vifuatavyo;
Nyuzi 3 o 0045-31 o 00' Mashariki mwa Greenwich na nyuzi 1 o 00-3 o 00'
kusini mwa Ikweta. Ipo milimita 1200 juu ya usawa wa Bahari. Hali hii
inafanya Halmashauri ya Wilaya Bukoba kuwa na misimu miwili ya mvua
yaani Vuli ambayo huanza mwezi Septemba na kumalizika mwezi Desemba na
masika ambayo huanza mwezi Machi na kumalizika mwezi Juni. Kipindi cha
Julai hadi mwanzoni mwa mwezi Septemba ni kiangazi na kipupwe uanza
mwezi Januari hadi mwezi Februari.