Bukobawadau

RATIBA YA VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE KUANZIA TAREHE 26 MACHI – APRILI 5, 2012


Taarifa inatolewa kwa Umma na Wadau wote kuwa Vikao vya Kamati za Bunge zimeanza shughuli zake kuanzia 26 Machi na vitaendelea hadi tarehe 05 Aprili 2012, zikiwamo ziara za baadhi ya Kamati nje ya mkoa wa Dar es Salaam kama Ratiba inavyoonekana hapa chini.

Miswada miwili ya Sheria inategemewa kusomwa kwa mara ya pili katika Mkutano ujao wa Bunge. Kwa ajili hiyo, Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji itasikiliza maoni ya wadau juu ya Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Mwaka 2011 (The Livestock Institute Act, 2011). Wakati huo huo, Kamati ya Maendeleo ya Jamii itasikiliza maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Hifadhi ya Jamii (The Social Security Law, 2011).

Wananchi wote kwa ujumla na Wadau wanaalikwa kushiriki katika vikao hivi ili waweze kutoa maoni na ushauri wao kwa ajili ya kuboresha Miswada hiyo. Vikao vyote hivyo vitafanyika Siku ya Jumanne Tarehe 27 Machi 2012 kwenye Ofisi Ndogo ya Bunge, Jijini Dar es Salaam, Kuanzia saa 3:30 asubuhi.

Imetolewa na:

OFISI YA BUNGE;IDARA YA ELIMU KWA UMMA, HABARI NA UHUSIANO WA KIMATAIFA


Next Post Previous Post
Bukobawadau