USAFI WA MAZINGIRA WAZIDI KUIMARIKA PEMBEZONI MWA ZIWA VICTORIA.
Sera ya sheria ya usimamizi wa Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 imeendelea
kutekelezwa katika mkoa wa Kagera.Katika utekelezaji wa sera na
sheria,Mkoa uliandaa mpango shirikishi jamii wa hifadhi ya mazingira.
Mpango huu unaainisha uhusiano uliopo kati ya uharibifu wa mazingira na
umaskini uliokithiri kwa sababu maliasili kama vile ardhi,misitu na
vyanzo vya maji;ambazo hutumika katika uzalishaji huharibiwa na
kushindwa kutoa tija inayokusudiwa na hivyo kukwamisha juhudi za
wananchi kufikia lengo la maisha bora kama ilivyo katika Dira ya Taifa
ya maendeleo (2025)
Mikakakti ya
utekelezaji wa mpango wa hifadhi ya mazingira ya ziwa vixtoria
iliyotekelezwa katika kipindi hiki na kutoa Elimu kwa wadau wa ziwa
Victoria kwa kupitia semina na makongamano ya wavuvi, viongozi wa
Serikali,Viongozi wa asasi zisizo za Kiserikali,wamiliki wa vyombo vya
usafiri wa maji,na jamii iliyo kando kando ya ziwa Victoria.
Taasisi ya
uangalizi na uendelezaji wa ziwa Victoria (LVFO) kwa kushirikiana na
wadau wengine wa ziwa Victoria wamesaidia kutekeleza mkakati kabambe wa
Mkoa wa kuunda na kuwezesha vikundi vya ulinzi wa Rasilimali na
usimamizi shirikishi wa Rasilimali ikiwa ni pamoja na dhana ya
ujasiriamali na kuinua kipato cha wananchi kwa kutumia ziwa Victoria
bila kuathiri mazingira.
Bustani safi zenye Viti vilivyo jengewa pembezoni mwa Ziwa Victoria hakika mazingira yanapendeza.
Na hii ndio sehemu itakpofanyika Birthday ya Mwaka Mmoja wa Libeneke la Bukobawadau
Hali kama hii ya kijana huyu aliye kutwa na Camera yetu amejilaza mchangani/ufukweni Bukobawadau tunaona ni mojawapo ya changamoto kwa Manispaa na wasimamizi au walinzi wa maeneo haya.