Bukobawadau

WADAU WATUNUKIWA VYETI VYA UJASILIAMALI KATIKA SEMINA YA MWISHO NA MAFUNZO YA KUKUZA KIPATO

Ndg Kisimba akifunga rasmi semina ya wajasiliamali kwa niaba ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Akiongea na Wajasiliamali ndg Kisimba amegusia hali ya ushindani wa Biashara na kuwataka Wadau kuakikisha wanakwenda sambamba na Ushindani wa ajira na Biashara katika soko la pamoja la jumuia ya Afrika Mashariki.
Mdau Wilbroad G.Mtabuzi akitoa mada kwa wajasiliamali juu ya  Siri ya utajiri, namna ya kuanzisha biashara,namna ya kutafuta masoko,namna ya kupambana na vikwazo kwenye biashara na mwisho kaongea namna ya kutunza  kumbukumbu za hesabu.
Ndg Chief  Diwani Kijana wa Kata Kahororo ndani ya Manispaa ya Bukoba amesema Kijana anapokuwa hana kazi ya kufanya anaona ni bora ajiunge katika makundi yanayotumia dawa za kulevya ili apoteze mawazo jambo ambalo linahatarisha afya zao hivyo njia ya kumsaidia ni kumuelimisha kwa kupata mafunzo ya Ujasiliamali.
Katika Semina hii Wadau wote walioshiriki wametunukiwa Vyeti vya Ujasiliamali.
Kutoka kushoto anaonekana Bi Konso na mwisho kulia ni Mdau Valelian Mkurugenzi wa 90.5 Vision Fm Radio.
 Swala zima la kukuza kipato limemgusa kila Mdau.
Bi Matrida Meneja wa 90.5 Vision Fm Radio akijaribu kutoa hoja yake.
Hatua ya kufanya majaribio ya kuchanga sabuni za magadi,na mafuta ya kujipaka.
 Mafunzo yametolewa kwa nadharia na matendo,pichani inaonekana ndoo ya SHAMPOO ikiwa tayari kwa matumizi!!!
   Kwa hivi sasa swala la Ujasiliamali linapewa kipaumbele kote nchini.
Hakika somo linaonekana kueleweka kwa washiriki wote kama wanavyo onekana katika hali ya tabasamu.
BUKOBAWADAU BLOG TUNATOA PONGEZI KUBWA KWA KAMPUNI INAYOTOA MAFUNZO YA UJASILIA MALI KUWEZA  KUFIKA BUKOBA NI GESAP CO.LTD NA DIMOD INTERGRATED SOLUTIONS&AWARENESS YA JIJINI DAR ES SALAAM !!!!!!!!Next Post Previous Post
Bukobawadau