Bukobawadau

MKOA WA KAGERA WAANZISHA SIKU YA MIGOMBA DUNIANI BAADA YA MIAKA 750 TANGU ZAO LA MGOMBA KUWEPO DUNIANI


Mkoa wa Kagera waasisi siku ya migomba duniani tangu zao la mgomba kuwepo hapa duniani zaidi miaka 750 iliyopita. Siku hiyo ya migomba duniani imeadhimishwa kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Kagera  Kijiji cha Rusumo na Kata ya Rusumo Tarafa ya Nyamiaga Wilayani Ngara  tarehe 19/4/2012 na kuhudhuriwa na wakulima wa ndizi kutoka mkoa mzima wa Kagera na Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma.

Mgeni rasmi siku hiyo ya Migomba duniani alikuwa Mhe.Kanali Mstaafu Fabian I. Masswe pia nchi wafadhili wa kilimo cha migomba ya kisasa Ubelgiji iliwakilishwa na Prof.  Swinenon ambaye ndiye mvumbuzi wa migomba ya kisasa ya PHIA ambayo kwasasa inastawi vizuri Mkoani Kagera na Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.

Mratibu wa mradi wa migomba Kagera Mugenzi Byachwezi aliwashukuru serikali ya Ubelgiji inayoongozwa na mfalme kwa kufadhili mradi wa migomba Kagera kwa zaidi ya bilioni 120 fedha za Tanzania tangu mradi ulipoanza mwaka 2009 mpaka sasa.

Aidha Bw. Byabachwezi aliiomba serikali ya ubelgiji kuendelea kufadhili mradi huo baada ya muda  wa mradi kumalizika mwaka 2013 ili kumalizia baadhi ya vipengere vya mradi ambavyo vitakuwa havijakamilika kwa muda huo, mfano; kuanzisha kituo cha taarifa mbalimbali za kilimo cha mgomba mkoani Kagera.

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe katika hotuba yake aliwaomba mradi 
wa migomba kuanza kusistiza zaidi uzalishaji wa ndizi kwa wakulima lakini pia na kuendelea  kusambaza mbegu bora za migomba. Pia kuendeleza kutoa elimu juu ugonjwa wa migomba uitwao unyanjano unaoishambulia migomba na bado haujapata dawa.

Pia Mhe. Massawe aliwasistiza wananchi kuendeleza kilimo cha ndizi na kuzalisha ndizi kwa wingi kwa ajil ya  chakula na biashara na kuacha kilimo cha kuchumia tumbo. Aidha aliwahakikishia wakulima kuwa serikali inafanya juhudi za kutafuta masoko kutoka sehemu mbalimbali duniani ili zao la ndizi lipate bei nzuri itayomkombao mkulima.

Mwisho Mhe. Massawe aliishukuru serikali ya Ubelgiji kuuona mkoa wa Kagera na kuupa 
ufadhili katika kilimo cha migomba ili kuinua kipato cha wananchi wake. Pia aliwashukuru viongozi wa mradi wa migomba Kagera  kumkaribisha  kuwa mgeni rasmi na yeye kuwa muasisi wa siku ya migomba duniani, “Nimevunja rekodi ya dunia na rekodi yangu mwenyewe kwa kuasisi siku ya migomba duniani.” Alimalizia Mhe. Massawe.

 
Siku hiyo ya migomba Duniania iliambatana na kutembelea mashamba ya kuzalisha mbegu na  kusambaza, pia mshamba ya kuzalisha ndizi Wilayani Ngara. Aidha wakulima kutoka kila wilaya katika mkoa wa Kagera waliweza kuonyesha bidhaa mbalimbali zinazotokania na zao la ndizi. Pia wakulima na wajasiliamali walipewa elimu juu ya kudhibiti ugonjwa wa unyanjano katika mashamba yao ya ndizi.

Na:     Sylvester Raphael,
            Afisa Habari Mkoa,
       KAGERA
Next Post Previous Post
Bukobawadau