Bukobawadau

MKOA WA KAGERA WAPATA USAFIRI NA VIFAA VYA KUKUSANYIA TAKWIMU ZA KILIMO VIJIJINI.

MKOA WA KAGERA WAPATA USAFIRI NA VIFAA VYA KUKUSANYIA TAKWIMU ZA KILIMO VIJIJINI.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Akabidhi pikipiki nane kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba kwa ajili ya kukusanya taarifa na takwimu mbalimbali za kilimo kutoka  vijijini katika Mkoa wa Kagera.
Pikipiki hizo zimetolewa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ikishirikiana na shiririka la Kimataifala Uhusiano la nchini Japan (Japan International Cooperation Agency, (JICA)   ambalo limewakilishwa na Bi. Akasaka Kyoko wakati wa kukabidhi  pikipiki hizo nane.
Mhe.  Massawe pia amewasistiza sana Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa kutunza pikipiki hizo na kuzifanyia kazi iliyokusudiwa na si vinginevyo. Aidha aliwaomba maafisa kilimo watakaozitumia pikipiki hizo kukusanya takwimu za kweli ili kuondokana na tatizo  takwimu zisizo sahihi.
Pamoja na pikipiki hizo na JICA pia waliendesha mafunzo ya ukusanyaji takwimu na kugawa kompyuta moja na mfuko wake, na Flashi mojamoja kwa kila Halmashauri ya wilaya na manispaa kwa ajili ya kukusanya na kutunza takwimu za kilimo vijijini.
Mkuu wa Mkoa aliwashukuru JICA kwa kujitolea kuleta maendeleo Tanzania na hasa katika mkoa wa Kagera. Ambapo pia amewahakikishia JICA kuwa serikali itaendelea kuhamasisha wananchi kuondokana na kilimo cha kuchumia tumbo na kujikimu na kuhamia katika kilimo cha biashara zaidi.

Na: Sylvester Raphael
AFISA HABARI KAGERA

Pikipiki Nane Ambazo Zimetolewa kwa Mkoa wa Kagera Kutoka Serikali ya Tanzania Kupitia Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ikishirikiana na JICA Kutoka Nchini Japani
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Katikati Akiwaasa Wakurugenzi  wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kuzitumia Pikipik hizo kwa Kusudi lililokusudiwa.
 Mhe. Massawe Akihakikisha kweli Pikipiki hizo kweli ni mpya na zipo tayari kwakufanya kazi vijijini.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Akikabidhi Pikipiki kwa Wawakilishi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa.
 Mkuu wa Mkoa Akimshukuru Bi. Akasaka Kyoko Mwakilishi wa Shirika la kimataifa la Japani (JICA) kwa ufadhili wa Pikipiki za kukusanya Takwimu za Kilimo vijijini

Picha zote na Afisa Habari Mkoa.Next Post Previous Post
Bukobawadau