Bukobawadau

MKUU WA MKOA MH. MASAWE ATOA SHUKURANI KWA KAMPUNI YA BIA YA (TBL) KATIKA UZINDUZI WA MUONEKANO MPYA WA BIA YA BALIMI.

Mgeni  Rasmi wa hafla hii Mh.Fabian Masawe akiongea na Wadau wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na Wageni waalikwa.
 Mh. Masawe amesema;Napenda niwaambie viongozi na wafanyakazi wote wa TBL kuwa sisi watu wa kanda ya ziwa Tunawapongeza na kuwashkuru kwa kutambua umuhimu wetu hadi wakatutengenezea Bia kwa heshima yetu,Bia ambayo inapatikana kanda ya  Ziwa tu na zaidi ya yote wakaipa jina linalotambulisha hasa katika shughuli kuu ya Kanda hii yaa "BALIMI"ikimaanisha "WAKULIMA"

Pamoja na kutupa heshima hiyo, Bia ya Balimi pia imekuwa na mchango mkubwa sana katika kanda yetu kufatia mambo mbalimbali inayofanya kwa jamii;hii ni pamoja na;
  • Kudhamini mashindano ya Ngoma za asili za Kanda ya ziwa-hii inatusaidia kukumbuka na kudumisha mila na desturi zetu.
  • Kudhamini mashindano maarufu.ambayo wengi tunayapenda,haya si mengine ila ni Mashindano ya Mitumbwi,nina hakika haya ndio mashindano ya kuvutia zaidi katika kanda yetu-Hongereni sana.
  • Pia wanadhamini Tamasha la kuendeleza na kudumisha Mila na Desturi za Mkoa wa Tabora.Tamasha hili linajulikana kama "Tamash la Mtemi Mirambo". 
Anaonekana Mdau Ndg Katumwa kufutiwa na JAMBO kutoka kwa Mkuu wa Mkoa.
Mdau Philpo na  Chinga Evody ni sehemu ya Wageni waalikwa.
Mwanaharakati Mzee Kabugumira ikiwa ni mda mrefu atujakutana.
 Muwakilishi wa TBL akimkaribisha Chakula Mgeni rasmi.
 Chakula hiki kimeandaliwa na Hawa Mabruki(Mama Hassan)
Wapili ni afisa utamaduni Manispaa ya Bukoba Ndg Rugeiyamu.
 Waalikwa wakiendelea kupata huduma ya Chakula.
Wadada hawa ni  wa kundi la burudani la TBL
Anaangalia kinacho Bi Sima Isaya.
MC wa shughuli akitoa nafasi kwa Kundi laburudani la Kakau Band
 Mpiga Dram wa Kakau Band ya Mjini Bukoba.
Wanenguaji wa Kakau Band.
Shughuli ya Uzinduzi wa muonekano mpya wa Bia ya Balimi wazidi kupamba.
Kundi la burudani la ICL likiwasha moto.
Ni siku ya kuburudika na Bia ya Balimi hafla hii imefanyika Usiku wa Jana kwenye Ukumbi wa Hotel ya Coffee Tree Inn.



INAENDELEA SOOON.... !!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau