Bukobawadau

BUGANGUZI ,KAGONDO ,KAMACHUMU HII LEO

Ukifika kijiji cha Buganguzi  Muleba ni  tofauti kabisa na kipindi cha nyuma  kwani migomba imeshambuliwa sana na baktelia na kuleta ugonjwa uitwaoMnyauko.
Picha ya Mgomba wenye Ugonjwa wa Mnyauko.
Baadhi ya wakulima wamekata tamaa na mashamba yao.
Kijiji hiki ndio Chimbuko langu Mdau Mc Baraka (Blogger)
Center maharufu kama (akona)
Nikalikita Mtaa wa Tibaigana ili niweze kupata  kumbukumbu
Kumbe Mzee mwenyewe yupo kijijini hapa na hii ndilo gari analotumia.
 Mzee Tibaigana kushoto akisalimiana na Mzee Galiatano.
Kuambiwa tu neno Bukobawadau ikalazimika picha ingine faster,na kushoto kabisa ni Uncle Tifu.
Katika kuweka usawa wa mambo na Wazee wangu ukizingatia fulsa kama hii ni mara chache kujitokeza.
Camera yetu ikiangaza Mji wa Kamachumu.
Moja kwa moja Nyumbani kwa Mzee Ali (AL-SAQRY)
Upendo kwa wazee wetu uko wazi, hivi ndivyo mzee Ali alivyomlaki Mzee Galiatano.
Masikani kwa Mzee Jaffary Kamachumu.
Hekaheka zinazoendelea katika Mji wa Kamachumu.
Ni kanisa la wakatoliki lilipo Kagondo,ndani ya jimbo la kaskazini Muleba.Kanisa hili lilijengwa na wamisiomari mwanzoni mwa 1880.Ikiwa ni pamoja na shule na vyuo .
Hospital ya Kagondo bukoba Catholic Diocese.
Kagera ni miongoni mwa mikoa iliobahatika kupata maendeleo makubwa kiuchumi na kijamii kabla na baada ya uhuru.
hii ote ni kutokana na wamisionari wa madhehebu ya Kilotheri na Wakatoliki walio ingia kagera miaka ya 1880 na kuazisha shule za msingi,sekondari na vyuo vya ualimu.
Ikiwa ni kabla ya kuonana na Uongozi tayari nimevutiwa na Usafi wa Mazingira kiujumla na siwezi kuongea chochote juu ya swala zima la huduma kwa sababu nila kitaalam japo wanasifika katika tasnia ya Vipimo.
Nakutana na Afisa utawala wa hospital hii   Ndg Josue Joseph  ili niweze kupata ruksa ya kuchukua picha mbalimbali na kuongea nae maswala  mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutaka kujua changamoto zinazowakabili.
Niliweza kuelekea wadi za private na kumwona Mgonjwa niliyemfahamu kwa Jina la Mzee Manuel Blasio hakika hali yake si njema  nimwombee dua zenu wadau.
Mwonekano wasehemu ya Mapokezi.
Zaidi kuhusiana na hospital hii tembelea www.kagondohospital.com
Next Post Previous Post
Bukobawadau