Bukobawadau

HAPA NA PALE NA CAMERA YETU PANDE ZA RUSUMO NGARA NA NCHI JIRANI YA RWANDA

Haya ni maporomoko ya maji Rusumo falls,tetesi  kubwa ni kwamba  maongezi yapo ukingoni kwa nchi wahisani kuja kufua umeme na kuleta neema kwa Tanzania,Rwanda na Burundi maana mita ya nchi hizi ndio inaungana na kuleta hali hii na hakika dalili za kupata umeme  zipo.

 Na kasi ya haya Maji BUKOBAWAWADAU BLOG hatujawahi kuona hapa ni upande wa daraja la Rusumo boda.
 Ukivuka daraja hili upo nchi jirani ya Rwanda.
 Mto huu unatokea upande wa Tanzania kuingia kwenye hayo  maporomoko
Rusumo boda, mpakani mwa Tanzania na Rwanda.
Gari hii imekutwa porini tetesi zinasema ina kama miezi minnee tangu imepata ajali na mwenye nayo ni kama kaisusa...!!
 Hiyo Gari iligonga hapo pembezoni mwa uzio wa barabara hii  kuelekea Biharamulo.
Kazi ya Ujenzi wa Barabara unaendelea.
 Ndg Mdau ukibahatika kufika Kigali Rwanda hakikisha unafika hapa ni makumbusho mauaji ya  mwaka 1994 hakika chozi litakutoka...
Hapo mimi sisemi ila ni Mdau Deo Rugaibula na Kaka mkuu wakiwakilisha pia kupata fursa ya kujifunza,Shangaa mdau una mika 15 mkoani Kagera ata Mtukura hupajui.
Mdau Deo akiwa na wenyeji hapo Kigali katikati ni Mr Emmanuel Mgamage na Mrs wake ni wakarimu na mara kwa mara utembelea Bukoba yetu.
Ndani ya makumbusho, wanaonekana wadau na mwenyeji wao Mrs Emmanuel, Ukiwa nchini Rwanda ukajikana wewe ni Mtanzania unapewa heshima kubwa sana na hili sijui ni kwa nini?


Sehemu iliozikwa miili ya wenzetu kufatia mauaji.
Wanaonekana wadau hapa kila mtu anampiga fix(Uongo mwenzake ) wote nawaelewa vizuri
 Mji ni msafi mpaka raha, kwa habari za chini chini ni kwamba Mshauri wa Kagame ni Ton Blair.
Wakati muhafaka.
Kigali by Night, kwa mbali anaonekana ... MUHUSIKA akivinjali mtaani ila kubwa zaidi ni usafi Uwezi kuona ata kipande cha kucha  iliyokatwa na kiwembe.
Next Post Previous Post
Bukobawadau