Bukobawadau

HIVI NDIVYO ILIVYOKUA SHUGHULI YA KAPU LA MAMA (MJUBURO) KWA WANANDUGU AFIDH NA AZIZA

Mdau Hafidh na Bi Aziza   wanandugu hawa wakiwa katika pozy la pamoja  ikiwa leo ni siku yao ya kipekee kwa mzazi wao kuweza kutimiza adhima ya kuwafanyia shughuli ya kapu la mama maarufu kama (mjuburo)
Mama Mzazi wa Vijana hawa akitoa nasaha kwa wanae sambamba na kuwashkuru wadau waliojitokeza katika shughuli hii
Akiongea kwa umakini ,utulivu, busara na kwa hisia  Bi Aziza kikubwa alicho kisema ni  nani kama Mama hakika na akamshukuru Mungu...!!
Ndg na Jamaa wakifunguka kwa furaha  na ndelemo
Mambo yetu  yale kwa akina Mama, hapa illikuwa si mchezo ama kwa hakika Ukumbi wa Linas umetikisika.
 Weeeeee!!!!
 Wadau wakishangweka
Mwonekano wa watu mbalimbali waliojitokeza katika shughuli hii ya Kapu la mama ambapo Bi Azizi  anaolewa alikadhalika Kaka yake  Afidh yeye anatalajia kufunga  ndoa hivi karibuni mjini hapa.

 Katika hali ya kupendeza anaonekana Mdau Hafidh na  Wapambe wake waki bhampa side to side.
 Mama Aziza akiendelea kutoa  Zawadi mbalimbali.
 Mambo ya Jikoni yakitekelezwa na Mama Aziza.(hii kweli inahusu...)
Zawadi zikiendelea kutolewa na kupokelewa kama anavyo onekana Bi Selina katika ushirikiano  na Bi Aziza.
 Bukobawadau tunachukua fulsa hii kutoa pongezi kwa Wanandugu hawa na familia nzima ya Abdulmalick wa Kashai.
Watu kutokana pande mbalimbali wakiendelea kufatilia kinachoendelea.
Washereheshaji wa shughuli hii  walisimama vyema Bi Shamila wa Mashauzi wa 88.5 Bk Kasibante Fm Radio na Bi Joyce Lubozi maarufu kama(teacher) pichani.
Kushoto anaonekana Mama Sabrina Visram na Mama Seleda hawa ni wadau wakubwa wa shughuli hii.
 Mdau Shukru pichani akisema safi sana!!

Pongezi kutoka kwa Bi Joyce Lubozi
Mama mzazi katika picha ya pamoja na wanae.
Katika kupongezena kwa mchakato mzima..
Mdau Afidh aka Kigaisa.

INAENDELEA...
Next Post Previous Post
Bukobawadau