Bukobawadau

Bukoba Wadau tunakumbuka miaka 16 ya ajali ya 'MV bukoba.

Mei 21,1996 katika ziwa Victoria,Mwanza Tanzania meli ya Mv Bukoba ilipata ajali na zaidi ya watu 800 kupoteza maisha yao.Meli ilizama kilomita 30 kukaribia kutua nanga kwenye bandari ya mwanza ikitokea Bukoba.
Meli ikuwa na uwezo wa kubeba idadi ya watu 430. Kwenye first and second class orodha ya abiria ilikuwa 443 na kwenye third class hakukuwepo rekodi yoyote .Takribani 1000 walifariki kwenye ajali hiyo.

Mv Bukoba baada ya kugeuka chini juu.Hiyo sehemu yenye rangi nyeusi ni sehemu ambayo kawaida inakuwa chini ya maji .Walikuja watu(bila kujua wanafanya nini) walikata sehemu hiyo mbele chini yenye "ombwe" na kufanya kama pulizo lililotobolewa na meli ikazidi kuzama
Mnara wa kumbukumbu ya ajali ya Mv Bukoba,wenye orodha yabaadhi ya majina ya waanga wa ajali.Ukisimama eneo hilo unaweza kuona kwa mbali eneo ambalo Mnara umejengwa kwenye shule ya wasicha Bwiru jijini Mwanza.

Afrika ya kusini ilibidi kutoa msaada wa wanamaji wake waje kutusaidia kufanya uzamiaji wa kina kirefu kwani tulikuwa hatuna hivyo vifaa na utalaamu(sijui inagharimu kiasi gani kuvipata vifaa na utalaamu)

Inasemekana Meli ilikuwa na ubovu lakini iliruhusiwa kuendelea na kazi kama kawaida.(nani anajali au kuwajibishwa?)

Vifaa vya uokoaji mfano majaketi(life jacket) n.k na vitu kama hivyo vilikuwepo vya kutosha?( au hakuna uzembe wa viongozi..ni kazi ya Mungu kama walivyozoea kusema)

SWALI LA MSINGI!!!!!
hivi Serikali imeshindwa kutenga japo dakika 3 nchi nzima kusimama kuwakumbuka ndugu zetu waliotutoka kutokana na uzembe wa watendaji wa serikali?

Kama wanaweza kukusanya mamilioni kusherekea sherehe za kisiasa inagharimu nini kutoa tamko kuhusu hiyo siku.bukoba wadau tunawaomba wadau wote tutowe maoni.

Poleni sana wafiwa..tupo pamoja ..mwenyezi Mungu awapumzishe mahala pema peponi woote waliotangulia mbele ya haki.Amina
Next Post Previous Post
Bukobawadau