Bukobawadau

Maombi ya udhamini Tsh 25.8 Mil Zinahitajika kwa ajili ziara ya kujifunza kwa vitendo nchini Rwanda may 25-27 , 2012.


 Ndg mpenda maendeleo ya kagera

Kampuni ya Kiroyera tours kwa kushirikiana na mtandao wa www.audax-kagera.com imeandaa ziara maalum ya kwenda Kigali nchini Rwanda kwa siku tatu kuanzia May 25, mwaka huu itakayowashirikisha viongozi mbalimbali wa Serikali, ambao wataambatana na wafanyabiashara, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa na wadau mbali mbali.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe, ndiye atakuwa kiongozi wa msafara wa ziara hiyo, wewe kama mdau mkubwa wa maendeleo katika nchi hii unaombwa uwe mmoja wa wadhamini wa ziara hiyo muhimu, udhamini ni kwa ajili ya gharama za usafiri wa kwenda na kurudi, malazi, chakula, sare n.k.
Ziara hiyo inamalengo  yafutatayo;
·         Kuuwajengea uwezo mbalimbali viongozi na namna ya kuwahamasisha wananchi washiriki kikamilifu juu ya suala zima la kuhifadhi mazingira.
·         Pili Kuwajengea uzoefu wana Kagera kuelewa  na kufahamu fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana nchini  Rwanda hali itakayowawezesha kukabiliana na changamoto zilizoko ndani ya soko la pamoja la Afrika Mashariki
·         Wana Kagera kufanya utalii na kukuza uelewa wa utalii ikiwa ni pamoja na kurifresh ( leisure) kwa kumuunga mkono Balozi Khamis Sued Kagasheki Waziri wa mali asili na utaliii ambaye ameteuliwa na Rasi hivi karibuni
Ujumbe wa mkuu wa mkoa utakuwa na watu 65, ziara nzima inatarajia kugharimu shilingi milioni 25.8 ambayo inahusisha usafiri kwenda na kurudi, visa,  malazi ,Chakula, tours, matangazo, sare ( kofia, tshirts, tracksuit ) na mengineyo
Tunaomba mchango wako kabla ya tarehe 20th May 2012 na mchango wako upitie account no OIJ1056362800 CRDB BUKOBA

Kwa mawasiliano zaidi tafadhali wasiliana na Mratibu wa safari hii Bw. William Oswald Rutta kwa namba 0784 568276 au Audax Mtiganzi 0784 939586
Nimeambatanisha barua ya Mh. Mkuu wa Mkoa ya kukubali kuongoza msafara na pia muhimu unakaribishwa kushiriki ziara hii ya ki historia. Utakumbukwa kimkoa kwa mchmago wako na kuitangaza bishara yako
 
Kagera amani na maendeleo!!


Next Post Previous Post
Bukobawadau