Bukobawadau

MSAADA UNAHITAJIKA KWA MDAU LAUREN LAURENT MKAZI WA BIHARAMULO


Bukobawadau Blog tumeshuhudia mdau huyu katika hali hii na  akihitaji msaada  wa matibabu kwa  Mzee Raza wa Izaas Medical Project mjini hapa.
 Wao Izaas na shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kuwasaidia watu wenye shida na wenye magonjwa mbalimbali   na kutoa miguu ya bandia kwa watu wenye ulemavu.

Akiongea na Bukobawadau Mkurugenzi wa Izaas Ndg Raza Fazal anamesa "Takwimu zinaonyesha kuwa Wilaya za Chato na Biharamulo kuna wagonjwa wengi wa Goita na matatizo mbalimbali  hivyo walifanya mpango na kuagiza wagonjwa wapatao 20 kutoka Wilaya ya Biharamulo na wakati wanafika katika ofisi za Izaas Mjini Bukoba kulikuwa na Mgonjwa mmoja wa ajabu sana mwenye uvumbe kichwani ambae ni Ndg Lauren Laurent mwenye miaka 46.
Lauren alipata ugonjwa huu tangu  miaka ya sabini  na kwa kukosa msaada ndio maana hadi leo hii yupo katika hali hii,na tatizo linazidi kukuwa kila siku, na Izaas wamefanya jitiata na kumpeleka katika hospital ya Mugana na kukutana na Dr.Mazima ambae amekubali kuwa anaweza kufanyiwa Upasuaji(operation) pale pale Mugana.

Lakini Madaktari wengi walioko nje ya Nchi wameshauri kwamba ili Operation hii ifanyika panatakiwa awepo Neuron Surgeon(hii ni ngazi flani ya utalamu zaidi) akishirikiana na Dr. Mazima.

Mpaka tunaingia hewani tarifa kamili  ni kwamba Izaas wamefanikiwa kumpata Neuron Surgeon Dr. Nice Rutabasibwa wa muhimbili hospital na amekubali mgonjwa apelekwe pale.
Kushoto ni Mubarak Abdullah project Manager wa Izaas .
Kwa sasa mgonjwa huyu anahitaji msaada wa Nauli yake yeye na Dr. Mazima wa Mugana,pia gharama za Operation, vipimo vya MRI na matumizi yake akiwa Jijini Dar es Salaam
Kwa mawasiliano zaidi Email izaasmedicalproject@gmail.com AU Simu namba +255714533430 
Next Post Previous Post
Bukobawadau