Bukobawadau

kiroyera tours yapeleka wanafunzi wa bkb secondary serengeti

 Katikati ni Meneja wa Kampuni ya Kiroyera Ndg Wiliam Rutta akiwa na wanafunzi wa Bukoba sekondari
Katika kukuza Utalii wa ndani kampuni ya Kiroyera Tours imeamua kutoa offer ya kuwapeleka bure Wanafunzi wawili na Mwalimu mmoja kutoka Shule ya Bukoba Sekondari  kwenye safari ya siku nne ya serengeti na ngorongoro.

Ziara hii imeanza tangu 24 Juni hadi leo hii 27June ikiwa wameunganishwa na wanafunzi kutoka marekani katika chuo kikuu cha Minessota ( Biology Without Borders) ambao pia ni shule rafiki ya Bukoba Secondary. Pamoja na Kampuni hii kuwaleta wageni mbali mbali wanaochangia shughuli za kijamii mbali mbali ikiwemo watoto Yatima baadhi wanalipiwa karo za shule za secondary, wageni wengine wamechangia kwenye walemavu wa BUDAP kwa kununua bidhaa zao, wageni wengine toka nje wamesaidia Mugeza shule ya maalibino nk. Pia watalii wamekuwa wakichangia kwa kutoa ajira kwa watu mbali mbali wanofanya kazi katika kampuni hiyo.

Meneneja wa Kampuni hii Bw. William Rutta akijulikana sana kama Willy Kiroyera  ameamua kutafuta mabalozi wa kampuni hii kwa kuwalipia gharama zote ikiwa usafiri, kulala, chakula, gharama zote  kwa wanafuni wawili ambao ni Elizabeth John kidato cha sita , na Najim Guram wa kidato cha pili pamoja na mwalimu wao wa Computer Bw Majid Ally. Hata hivyo mwezi ulipita Kampuni hii iliwapeleka wanfuniz 46 kutoka chuo cha utalii Ntoma kujifunza kwa vitendo na wanafunzi wawili wa Shule za msingi mmoja kutoka Zamzam na Happy medium school
Mdau Mwalimu Majid akiwa na wanafunzi wake.

Sababu kubwa ni kuwaonyesha waone uzuri wa safari za mbugani na kutambua  pamoja na kujifunza na pia baadae kuwa mabalozi wa Kiroyera Tours katika kukuza utalii wa ndani na kumuunga mkono Waziri wa mali asili na Utalii Balozi Hamis  Kagasheki.

Next Post Previous Post
Bukobawadau