TAARIFA KWA WADAU WOTE WA MKOA WA KAGERA
Wapendwa Wana-Kagera,
Napenda kuwafahamisha kuwa kesho Ijumaa, tarehe 29/06/2012 mnamo saa 10:30 jioni, Wana-Bukoba, B'mulo, Karagwe, Muleba, Missenye na Ngara watakutana pale Bamaga-Golden Tree Bar, iliyopo Mkabala na Gate la kuingia Chuo cha Ustawi wa Jamii-Sinza.
Mkutano huu usiokuwa na itikadi za kisiasa wala mlengo wa kidini au ukanda ndani ya mkoa wa Kagera, utajikita katika kutafuta suluhu ya wapi Mkoa wetu umekwama na nini kitendeke ili ustawi wa mkoa na watu wetu uweze kurejea. Kamati iliyohusika na Maandalizi ya Mkutano huu itahakikisha washiriki wanapewa uhuru wa kuchangia kwa upana wa mada na kujitolea katika kutekeleza maazimio yatakayofikiwa.
Kwa ujumbe huu Bukoba Wadau mnaalikwa kuhudhuria pasipo kukosa. Ni matumaini yetu kuwa mtaisaidia Kamati ya Maandalizi kwa kusambaza mwaliko huu kwa Wana-Kagera Wengine.
Kwa niaba ya Kamati ninatanguliza shukrani kwa msaada wenu wa kusambaza ujumbe huu na kunuiya kuhudhuria mkutano.
Iwapo mtu atakwama kwa namna yoyote kufika eneo la mkutano basi awasiliane na Bw. Rutta 0717-310-538
Wenu katika kufufua Maendeleo ya Mkoa wa Kagera,
Erick M. Kimasha
BUKOBAWADAU
Bukoba Wadau ni mtandao unao toa habari na matukio yanayo tokea katika mji wa bukoba pamoja na mkoa wa kagera kwa ujumla.
Email:bukobawadau@gmail.com | Phone :Mc baraka:0784 505045, 0754 505043
Instagram @bukobawadau | Facebook @bukobawadau