Bukobawadau

TUNAKUJA TENA NA KIPENGERE KIPYA CHA MAISHA YA WATU MAHARUFU.

Hivi ndivyo ilivyokua  kwenye harusi ya Mke wa sita wa Rais wa Afrika ya Kusini  Jacob Zuma mwishoni mwa mwezi wa 4 .2012
Matukio yakiendelea katika harusi ya kimila.
Rais Zuma akiwa amevaa  Ngozi ya Chui na kubeba Ngao katika harusi ya kimila.
 Rais Jacob Zumana mkewe Bi Bongi Ngema wakikata Keki.
Wakitabasamu kwa pamoja.
Rais Zuma mwenye umri wa miaka 70 akiendeleza Ubishi.!!!

Msimamizi wa ndoa hiyo alikuwa ni mke wa nne wa Zuma aitwaye Nkandla katika sherehe iliyofanyika KwaZulu-Natal na kufuatiwa na sherehe za kisasa ambazo zilikuwa ni pamoja na kukata keki.
Zuma na Ngema wana mtoto wa miaka saba wa kiume. Ndoa hiyo ni ya tatu katika miaka minne iliyopita naya pili tangu ashike urais wa nchi hiyo mwaka 2009 akiwa rais mwenye wake wengi.
Kiongozi huyo ameoa mara sita na ana watoto 21 ambapo mmoja wa wake zake amekufa na mwingine ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Nkosazana Dlamini-Zuma – ametalikiana naye. Wanawake hao hufaidika kwa kusafiri na rais huyo na kufanya kazi za ukatibu mahsusi, pamoja na kufuatana naye katika ziara za kiserikali.
Pamoja na kwamba Zuma aligharimia ndoa hiyo yeye mwenyewe, serikali pia imeongeza bajeti yake maradufu kwa zaidi ya Dola milioni mbili kutokana na kumwoa mwanamke huyo akiwa mmoja wa familia yake.
Hata hivyo, ndoa ya wanawake wengi inaonekana kupoteza umaarufu nchini Afrika Kusini ambapo ustaarabu wa nchi za Magharibi unazidi kuota mizizi ambapo idadi kubwa ya watu wa nchi hiyo hawakubaliani na utamaduni huo hivi sasa.


KIPENGELE HIKI CHA MAISHA YA WATU MAHARUFU KITAKUWEPO MARA MBILI KWA KILA MWEZI.


Next Post Previous Post
Bukobawadau