Bukobawadau

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA AUTEMBELEA MKOA WA KAGERA.

Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Bi Diane Corner Akiongea na Vijana Waliokuja Kujitolea Katika Uzinduzi wa Mradi wa VSO Kwenye Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe Akiongea na Balozi wa Uingereza Bi Diane Corner na Ujumbe Wake Mara Baada ya Kuwasili Mkoani Kagera na Kufika Ofisini Kwake Kumsalimia.
 Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe Mradi wa VSO Rasmi Mkoani Kagera kwa Kurusha Maputo Juu
 Palipo na Mama Hapakosi Baba, Huyu ni Mme Wake Balozi Diane na Mtoto Wao wa Kike
 Vijana Kutoka Nchini Uingereza Waliokuja Nchini na Mkoani Kagera Kuja kujitolea Wakimsililiza Balozi Diane Corner.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba Pamoja na Katibu Tawala Msaidizi Utawala (mbele) pia na Vijana wa Kitanzania ambao watajitolea katika Mradi wa VSO Wakimsikiliza Balozi Diane.
 Picha ya Pamoja Balozi na Mkuu wa Mkoa na Wajumbe Wote Walioshiriki Katika Uzinduzi Mradi wa Kujitolea wa VSO Mkoani Kagera.


Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi Diane Corner autembelea mkoa wa Kagera na kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa. Balozi Diane Corner alifika jana tarehe 05/07/2012 saa tatu asubuhi na kufika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa kumsalimia Mkuu wa Mkoa.

Akiongea na Mkuu wa Mkoa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Diane Corner alisema kuwa hiyo ni mara yake ya kwanza kufika mkoani Kagera na ni ziara yake ya kwanza katika mkoa huu.

Balozi Diane Corner tangu jana tarehe 05/06/2012 alianza ziara yake katika mkoa wa Kagera na kutembelea sehemu mbalimbali pia anaendelea kutembela sehemu hizo mfano Kemondo, na Chuo Kikuu cha Josia Kibira katika Halmashauri ya Wilaya Bukoba.
Pia atatembelea kikundi cha KAVIPE Kamachumu, Hospitali ya Kagondo Wilayani Muleba pia atatembelea Ishozi kwenda kuzindua siku ya Demora Wilayani Missenyi. Aidha tayari ameshiriki na Mkuu wa Mkoa katika kuzindua mradi wa Volunteer Service Organisation Tanzania (VSO).
Mradi wa VSO unaendeshwa chini ya Huduma ya Uraia wa Kimataifa (International Citizen Service, ICS), chini ya Mkurugenzi wake Tanzania Bw. Jean Van Walter. Mradi huu unahusisha vijana kujitolea kufanya kazi za kijamii, pia mradi huu umezinduliwa kwa mara ya kwanza mkoani Kagera lakini upo Tanzania nzima.
Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliwashukuru vijana wa Uingereza waliokuja kujitolea mkoani Kagera kuwa wataamsha chachu ya watanzania walio wengi kujifunza kujitolea. “Wakati wa Mwalimu Nyerere moyo wa kujitolea ulikuwepo mkubwa lakini kwa sasa umekufa, sasa vijana watajifunza.” Alisema Mhe. Massawe.
Balozi wa Uingereza Bi Diane Corner atajionea mambo mbalimbali ambayo alisema kuwa ana hamu ya kuyaona mkoani Kagera kama Kahawa, Maharage, Chai, pamoja na senene. Aidha Bi Diane Corner ameambatana na mme wake pia na mtoto wake wa kike, na anatarajia kukaa mkoani Kagera kwa siku nne tangu Julai 5, 2012.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael,
Afisa Habari Mkoa,
Kagera.
Next Post Previous Post
Bukobawadau