Bukobawadau

MASHINDANO YA MCHEZO WA POOL TABLE YANAYODHAMINIWA NA SAFARI LAGER YAZINDULIWA RASMI MJINI HAPA.

Mwenyekiti wa chama cha Pool Table Mkoani Kagera Ndg Samora Lyakura akiongea na makapteni wa timu zitakazoshiriki mashindano ya haya na kutoa ufafanuzi wa ratiba na  kupanga makundi.
Mashindano haya yatakayofanyika kwa siku 3 kuanzia tarehe 5-8 ambapo jumla ya timu  7 sitashiriki.
 Mgeni Rasmi Mh. Ibrahimu Idd Mabruk  diwani wa kata ya Bilele yanapofanyikia mashindano haya akiongea na washiriki.
Ndg James Magoli  msimamizi wa mashindano haya kutoka Intergreted Promotions & Communications kwa kushirikiana na Safari Lager.
 Kikubwa katika uzinduzi huu ni kupanga makundi ya timu zitakazon shiriki ambapo jumla ya timu saba zitashiriki katika makundi mawili, Kundi A litakua na timu 4 na Kundi B litakua na timu 3.
 Mechi zimepangwa kwa kuchezesha bahati nasibu,Pichani anaonekana Ndg Charles Karugira kapteni wa Mnyonge Pool Cener  akichagua karatasi ya timu ipi akutane nayo!!
Vivyo hivyo kwa kapteni wa Bukoba Pool Center Mdau Geofley John.
 Mzazi Samora akitekeleza jukumu lake kwa umakini kabisa!!!
Ratiba ilivyosimama  mchezo wa kwanza utazikutanicha timu za Q bar na Bilele Pool Center.
Msimamizi wa Mchezo huu Ndg James  Magoli akikabidhi vifaa vya mchezo kwa Mgeni rasmi.
 Mwenyekiti wa marefaree Ndg Eladius Lugalinda
Kapteni  Kelvin Wales wa Hamugembe akipoka posho kwa ajili ya Chakula.
Vyombo mbalimbali vya habari vimeshiriki kikamilifu.
Mpango mzima uko hivi na uwanja utakao tumika katika mashindano haya ni Q bar iliopo mtaa wa Lumumba kata ya Bilele.
Next Post Previous Post
Bukobawadau