Bukobawadau

MCHAKATO WA UKUSANYAJI WA MAONI YA KATIBA MPYA WAENDELEA MJINI HAPA.

Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katika akifafanua jambo juu ya awamu ya kwanza ya mkutatano wa kukusanya maoni ya wananchi.
 Wadau wakiwa katika mstari tayari kwa kutoa maoni yao yoyote yatakayojenga taifa letu.
Mdau Poroje na Patrick wakisikiliza maoni ya wadau mbalimbali
 Wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba wakitoa msaada kwa mlemavu wa macho ili aweze kutoa maoni yake
 Mlemavu wa macho akitoa maoni yake
Ustaadhi akitoa maoni yake juu ya mustakabali wa zanzibar ndani ya muungano na  swala  la mahakama ya kadhi.
Mdau akipata ufafanuzi wa namna ya kutoa maoni yake kwa njia ya barua.
 Wajumbe wa  tume wakipokea maoni ya mdau.
Mdau Salum Mawingu akitoa maoni yake juu ya migogoro ya ardhi iliopo na ardhi iwe dhamana kwa mmiliki na kutoa nafasi kwa taasisi za kidini mfano World Vision ziruhusiwe kuingia nchini ili kutoa huduma kwa faida ya wananchi .
Mkurugenzi wa Vision Fm Radio Ndg Valelean akiongea kwa  busara, umakini, utulivu na kwa hisia juu ya vipaumbele vyake,kikubwa alichokisema ni juu ya taasisi za kidini kulipa kodi kwani nazo zinafanya biashara.
Mdau akitoa vipaumbele vyake
Mdau pichani wakati akiendelea na maoni ikagundulika alishatoa hivyo akaambiwa asiendelee ila kikubwa alichokisema ni juu ya Ma Meya na wenyeviti wa halmashauri wasichanguliwe na Madiwani bali wapigiwe kura na wananchi wote.
Mzee Galiatano akitoa maoni yake mbele ya kamati ya ukusanyaji maoni , kikubwa alichokisema ni madalaka aliyonayoRais yapunguzwe  na asa  pale anapo mteua mtu aliyekataliwa na wananchi kuwa muakilishi popote.

 Mdau Mzee Philbart.
Mdau akisikiliza maoni ya wadau mbalimbali.
Wadau mbalimbali wakiendelea kusubilia kutoa maoni yao

Anaonekana Bi Janath Mussa na Familia ya Mwalia Peace wakiandika maoni yao.
Mzee Abdulziadi Kashinde akitoa maoni yake.
Wakiandika maoni yao kwa njia ya Barua.
 Ndg Simai Mohammed Said mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba akitoa angalizo.
Muamko ni mkubwa sana katika swalazima la katiba.
Mdau Abdul I shaq Bonge na Mdau Siraji wakitekeleza adhima yao katika mchakato unao endelea
Mlezi wa Bukobawadau Blogspt Ndg Peter Mugisha akijadili jambo na Mdau kikubwa ni ile hali ya ukali kwa wafanyakazi wa tume kitu kinachopelekea mwanchi kukosa amani wakati zoezi likiendelea.
Mdau Sued na Abibu pichani wakiongea na Bukobawadau wadau wamesema Swala la Serikali za Majimbo, Muungano,maswala ya mimba kwa wanafunzi ndio maoni yao makubwa japo wameshtushwa na kushangaza kuona maoni ya Dini yanakua  mengi kutoka kwa wadau mbalimbali kwao wanaona hii si dalili nzuri.
 Wadau maoni yakionekana kujirudia
Mwisho tunakuomba kupitia (Older Post)ILI kupata matukio ya MUDA MCHACHE uliopita na  kwa habari za papo kwa papo kwa kuuungana nasi kupitia  Facebook na Twitter @bukobawadau,@Dj cool Mc.Ndg Mdau kumbuka maoni yako ndio dira yetu katika kuendeleza libeneke hili mwisho kabisa  tunawatakia Waislam wote mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa RAMADHANI!!!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau