Bukobawadau

MABINGWA WATETEZI YANGA WAMEFUZU KUINGIA NUSUFAINALI YA KOMBE LA KAGAME 2012

 Pichani anaonekana mchezaji wa Yanga Yondani akichanja mbnga.

Klabu bingwa mtetezi Afrika Mashariki na Kati, Yanga ya Tanzania, imefanikiwa kuingia nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Kagame baada ya kuitoa timu ya Mafunzo ya Zanzibar kwa mikwaju ya penalti.
Matokeo hadi mwisho wa mchezo mjini Dar es Salaam siku ya Jumatatu yalikuwa 1-1, Mafunzo wakiwa wa kwanza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Ali Mmanga.
Yanga walifanikiwa kusawazisha dakika ya kwanza kipindi cha pili kupitia kwa Said Bahanuzi na kufanya mchezo uamuliwe kwa penalti baada ya dakika tisini, na Yanga kushinda kwa penalti tano kwa nne.
Yanga watacheza na APR ya Rwanda, ambao nao wametinga nusu fainali baada ya kuwatoa URA wa Uganda kwa mabao 2-1.
APR walipata mabao yao kipindi cha kwanza kupitia kwa Jean Claude Iranzi na Seleman Ndikumana, wakati bao la URA lilifungwa na Robert Ssentongo kipindi cha pili.
Kocha wa APR Mholanzi Ernest Bradnt anasema itakuwa mechi ya kulipiza kisasi; “Yanga walitufunga hatua ya makundi, hivyo tutahitaji kulipiza kisasi. Lakini pia tumeshinda kombe hili mara tatu nyumbani na sasa tunataka kulishinda ugenini, hapa Tanzania,” alisema.
Jumanne Simba itacheza na timu mpya kwenye mashindano haya, Azam, pia kutoka Tanzania, na Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo itacheza na Atletico ya Burundi.
Wachezaji  wa yanga wakiomba dua kabla ya mikwaju ya penati.
Wachezaji wa Yanha wakicheza hakunagana baada ya kuwatoa Mafunzo
Mfungaji wa Yanga ambaye kwa sasa ni mwiba ana goli sita pichani anaonekana aklishangilia  bao la kusawazisha dhidi ya Mafunzo.

 Mwisho tunakuomba kupitia (Older Post)ILI kupata matukio ya MUDA MCHACHE uliopita na  kwa habari za papo kwa papo kwa ungana nasi kupitia  Facebook na Twitter @bukobawadau,@Dj cool Mc.Ndg Mdau kumbuka maoni yako ndio dira yetu katika kuendeleza libeneke hili mwisho kabisa  tunawatakia Waislam wote mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa RAMADHANI!!!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau