Bukobawadau

WANAMEREMETAAA...WANAMEREMETA..!!!! NI HARUSI YA MDAU HAMIM SONGORO NA BI KHADJA AMIS ILIOFANYIKA HII LEO NYUMBANI KWAO KAMILABALA NA ITONGO KAMACHUMU

Maharusi Bi Khadja Hamis na Mdau Hamim Songoro  wa kamachumu wakiwa katika furaha  baada yashughuli iliyofanyika Nyumbani  Kamilabala na badae kuendelea kijijini Itongo Kamachumu.
 Nyumbani kwa Mzee Rajab Songoro mzazi wa Bwana harusi muda mchache kabla ya kuelekea Ukumbini kuendelea na  Maulid kwa Mzee Juma Lutende (Itongo)ndani ya Kamachumu.
Mdau Organizer ni mtu wa watu sana
 Wanaonekana  wa  Bwana Harusi
 Maharusi  wetu hivi ndivyo walivyochomoka kwa siku ya leo...!!!!tuwape pongezi vijana hawa..!!! Ukizingatia kuoa kuna mengi ndani yake na Mme ni tofauti na mwanaume "alikadhalika" kunatofauti kati ya  Mke na mwanamke najua wapo wachache wanaonisoma ni nini  namaanisha.!!
 Ninachoweza kusema kama blogger ni kwamba  raha ya maisha ni  siku ya harusi!!!!
Taswira ya mwanzo wa msafara wa maharusi wetu kutokea Sokoni Kamilabala kuelekea, Milama, hadi Itongo.
 Hivi ndivyo Mji wa Kamachumu ulivyo zizima kwa ndelemo,shangwe na vigelegele
Kwa ushirikiano wa familia ya Haji  Juma Lutende na familia ya Haji Rajabu Songoro  waandaji wa harusi ya Mdogo wao Hamim na Bukobawadau  tukitoa update papo kwa papo sasa tunajikita ITONGO ....!!!na kufikia hapa Matukio yatafuata taratibu kwani tunajaribu kutupia Video za harusi kupitia You tube..!!
 Kabla ya kuingia bandani  kitendo cha taratibu za kimila kimeanza kwa Bibi Harusi kukaa kwenye mkeka.
Katika hili wapambe ni mashuhuda.
 Utaratibu wa kuingia kibandani unaendelea...
 Hivi ndivyo alivyotokelezea Bw. Harusi  Mdau Hamim Songoro na mpambe wake Mdau Underson
 Baadaya maharusi ukuingia kibandani , ratiba ikaanza kwa dua ya ufunguzi

Sheikh wa Wilaya ya Bukoba Mjini  Sheikh Haruna Kichwabuta, na pembeni ni katibu wake Sheikh Ismairy.
 Ustaadh akisoma mlango wa kwanza wa Quran.
 Ustaadhi Abas akionyesha umahiri wa mlango wa pili.

Madarasat Kanazi ikiwatendea haki wadau waliohudhulia, na  utaweza kupata Video yake badae kupitia bukobawadau you tube.
Ni maulid ya harusi iliyohudhuliwa na watu wengi sana kutoka pande mbalimbali  na Nchi jirani  Uganda na Burundi.
 Razha ya kashida  iliyomithilika kutoka kwa Nazifa!!
Ustaath Dokt. Abas Byabusha akiwatunza waimbaji wa Qaswida.
 Anaonekana Mdau Ziada Songoro na wanamama wengine.
 Wanafamilia wakifuatilia kinacho kwa nyuma anaonekana Uncle Magimbi na Uncle Buruani  kwa mbele anaonekana Mdau Katete na Mdau Nuha wakiteta hili na lile.
Ikafika muda wa Bi Haruusi kutinga ukumbini ili kupata mawaidha kwa ukaribu kutoka kwa Sheikh Haruna
Ndipo nikashangazwa  na utundu wa Hamim.....!!!!faraha, tabasamu,jicho na pozy kuvionyesha kwa wakati mmoja hakika ni utundu usio wa kufundiswa.!!!!!
Bi Harusi Manshallah!!!!HAPA  nachukua fulsa hii kutoa pongezi zangu kwako Mdau Hamim na kuwapa pole wale akina fulani...  kazi kwao sasa na hapa wasema ni Mchina!!!!! LOL "watajibeba"


INAENDELEA..
Next Post Previous Post
Bukobawadau