Bukobawadau

HAPA NA PALE NA CAMERA YETU HII LEO PANDE ZA BANDARINI

Camera hii leo imezuka pande za Bandarini wengine upaita kastamu ekaheka tunakuta meli zaidi ya Victoria, ipo inayoshusha mzigo kutoka Kampala na kuna inayopakia sukari
 Mv Victoria kulia na FB Chacha mali  ya Kitana Chacha wa Mwanza ikiwa Kushoto
Meli ya FB Chacha na Orion ni mali ya Kamanga Ferry nayo inapakua mzigo kutoka Kampala.
Muda huo na Usafi unaendelea kwa ufupi ni full (kalibatano)hekaheka.
Mara nakutana na kundi la Wanafunzi kutoka  Wilaya ya Karagwe ambao waalimu wao hawajagoma wakiingia bandarini kujifunza baadhi ya mambo maana kibongo bongo mgomo ndio fashion.
Macaptain wa siku za mbeleni wakiingia melini
Mizigo iliyotoka  Mwanza
 Sukari kutoka kiwanda mama cha Kagera Sugar inapakiliwa melini kwenda Mwanza
Hekaheka za hapa na pale
Wabebaji katika mzuka.
Bandari ya Bukoba kama moja ya milango ya kuingia mkoani Kagera inahudumia Abiria na mizigo leo ijumaa ni siku ya ratiba ya Mv Victoria aka( kaitu kaila)
Mv Victoria ikipakua bidhaa ilizokuja nazo na badae kuanza kazi ya kupakia vya kuondoka navyo kwenda Mwanza kupitia bandari ya Kemondo
Mdau  Mama Ashura ambaye shughuli zake daima zipo bandarini akiwa katika pozi
Shule nyingi zimefungwa kupisha sensa hapa wanaonekana wanafunzi wa shule mbalimbali wanaokwenda  mwanza na mikoa jirani kwa likizo hiyo ndefu mpaka mwezi wa 9
 Ziara yangu bandari imenipa fursa ya kujua mengi sana, wafanyabiashara wakubwa  wanazidi kutambua umuhimu wa kuwa na bandari na kuitumia.
Uwepo wa Bandari kunatoa ajira kwa wana kagera,vijana wanapata mkate wa kila siku kupitia kubeba , malori yanapata kazi , yote juu ya yote bidhaa zinafika kwa gharama nafuu na bei inakua nzuri kwa wakazi wamkoa wetu kiujumla bei ya Kyamkwiki, Nyankele,Kaisho, Ruzinga haitofautiani sana na bei ya Izigo, Kemondo au Kyaka
Binafsi Mc Baraka Blogger nimejifunza  kua bandar ya bukoba inaweza kupokea na kutoa huduma kwa meli zaidi ya moja kwa wakati mmoja nimependa namna maofisa wa meli wakijitoa ile ile kuwafundisha wanafunzi wanaokuja kujifunza

BUKOBAWADAU BLOG  TUNAWAASA WADAU WOTE KUJIVUNIA ZIWA VICTORIA MAANA SI MIKOA YOTE YA TANZANIA YENYE FURSA  YA KUWA NA BANDARI KAMA HII SANASANA WANAJIVUNIA BANDARI ZA NCHI KAVU(DRY PORT) KAMA ILE YA ISAKA!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau