Bukobawadau

MAADHIMISHO YA MIAKA 100 TANGU IANZISHWE HOSPITALI YA KAGONDO

Bango la  matangazo ya siku ya kuadhimisha  miaka 100 ya  hospitali ya St. Joseph Kagondo , hospitali iliyoanzishwa mwaka 1912 ikiwa kama zahanati katika sehemu  ya Bushekya, nje kidogo ya eneo ilipo sasa.Hospital hii ipo kaskazini mwa mkoa wa Kagera na Magharibi ya ziwa Victoria  umbali wa nusu kilometa kutoka barabara  kuu ya Bukoba-Biharamulo.
 Askofu Mkuu Mteule Protase Rugambwa, katibu mshiriki wa propaganda Fide na Rais wa PMS(Pontifical Mission Societies)akiongoza maandamano.
Wanaonekana Mhashamu Askofu Method Kilaini, Askofu msaidizi wa jimbo la Bukoba,Mhashamu askofu Almachius Rweyongeza, Askofu wa Jimbo K atoliki la Kayanga kwa nyuma (kushoto)ni Mhashamu Askofu Nestor Timanywa, Askofu wa Jimbo  Katoliki la Bukoba.
Wafanyakazi waandamizi wa Hospital wakishiriki katika maandamano  ya Ibada.
 Wadau pichani anaonekana Mr Baganda, Mh Charles Mwijage Mbunge wa jimbo la Muleba Kaskazini(Mwenye Camera)Mh. Prof. Anna Tibaijuka, Mbunge wa Muleba Kusini na waziri wa Ardhi , Nyumba na Makazi, Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mh.Lembris Kipuyo na wa mwisho kulia ni Katibu wa CCM Wilaya Muleba Ndg Katalama.
Ibada ikiendelea
Mzee Baganda na Familia yake
Sehemu ya wanakwaya
Wadau wakiendelea na Ibada pichani ni Mh. Justus Magongo diwani wa kata ya Kagondo.
Tukio la kupeleka Vipaji
 Askofu Mkuu Mteule  Protase Rugambwa akipokea Vipaji
 Mashuhuda wa  kukata utepe na kubariki jiwe la  jubilei
Askofu Mkuu Mteule Protase Rugambwa akikata Utepe.
 Jiwe la miaka 100 ya Jubilei ya hospitali ya Kagondo  1912-2012
 Wanahabari na matukio.
Watumishi wa Hospitali ya Kagondo katika picha ya pamoja na Maaskofu.
 Mwanahabari wa ITV  Vedasto Msungu katika Exclusive na Mh. Mama Tibaijuka.


Wazo kuu katika jubilei ya Miaka 100 ya hospitali ya Kagondo.
  1. kumshukuru Mungu aliye mtendaji wa haya yote.
  2. kuwakumbuka na kuwaombea Maaaskofu, Mapadre, Mabruda na Wamisionari.
  3. Kuwakumbuka na kuwashkuru walioshiriki ujenzi wa hospitali hii toka zama za Misonge
  4. kutathmini maendeleo ya huduma ya tiba tangu mwanzo hadi leo na kuratibu miaka 100.
  5. kuwakumbuka na kuwaombea marehemu wafanyakazi waliotangulia.
  6. kuwaombea wafadhili,widhara ya afya, Viongozi wa Jimbo,na viongozi wa Chama na serikali
  7. kurekebisha na kuimarisha majengo na vifaa vya hospitali.
  8.  kumtaka kila mwenye uwezo wa kufanya kazi awajibike.

MWISHO TUSIKOSE KUTEMBELEA MTANDAO WA BUKOBAWADAU KILA SIKU KWA HABARI ZA UWAKIKA NA ZENYE TIJA PIA KUWAJULISHA WADAU WENGINE UWEPO WA LIBENEKE HILI YOTE JUU YA YOTE TUTOE PONGEZI KWA UONGOZI WA HOSPITALI YA KAGONGO JAMANI !!!!!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau