Bukobawadau

SALAAM ZA PONGEZI KWA MH. KAGASHEKI KUTOKA KWA ERICK KIMASHA

Wanajamvi,

Naomba kutanguliza samahani kwa wale nitakaowakwaza kwa kutumia au kuleta habari za kwenye blogs. La muhimu tukumbuke "Akakaikuru ke enshoni.....bakakaziika nkalola!"

Kupitia vichwa vya habari vinavyopatikana blog ya Mjengwa http://www.bukobawadau.blogspot.com  na magazeti mbali mbali nchini napenda kumpongeza sana Mh. Kagasheki. Hakika Jitihada, Ujasiri na Uzalendo wake, ni sifa kwetu Wana-Kagera.

Tukiwa na akina Om. Mwijage wanawakilisha kikamilifu toka backbenchers, tukawa na Mh. Mama Prof. na Mh. Kagasheki wanapokea na kufanyia kazi toka kingo zao, sifa njema ya Kagera itarejea kileleni. La muhimu ni kuwakumbusha kuwa ukarimu huanzia nyumbani. Na hivyo hizi jitihada zao ziendelee kwenda sanjari na utekelezaji wa mikakati ya maendeleo majimboni (nyumbani kwetu). Sisi wananchi tunachohitaji zaidi toka kwa Wabunge ni kuunganishwa na kushirikishwa kikamilifu katika kujiletea maendeleo. Na binafsi naamini hilo jukumu wanaliweza.

Tutabasiima kwiruka, bakabanza kulaba amalembo!

Mkolege.
Next Post Previous Post
Bukobawadau