Bukobawadau

KAPOTIVE Star Singers BUKOBA watoa album mpya

 Vol.4 Mama yetu
Kikundi mahiri cha KAPOTIVE Star Singers - Bukoba, kimetoa album mbili kwa mpigo, Vol: 4 inayoenda kwa jina la MAMA YETU, na Vol:5 inayoenda kwa jina la NAKUSHUKURU MUNGU.
 
Wakati anatoa taarifa hizi, Afisa masoko wa KAPOTIVE Star Singers amesema bado album hizi ni audio, na maandalizi ya Video yanaendelea kwa kiwango kizuri. Amesisitiza kuwa album hizi ni nzuri sana, na kila album ina nyimbo 12 ambazo ni nzuri ajabu kwa kusikiliza nyumbani na kwenye sherehe mbalimbali za kijamii.
 
Bw. Audax amesema album hizi kwa Bukoba mjini zitakuwa zinapatikana katika maduka ya 1- Mama wa Mkombozi 2- Gift shop 3- Church bookshop (Ujirani Mwema) 4- FM Studios.
 
Ikumbukwe kwamba toleo la kwanza la kikundi hiki inayoitwa Yesu ni Mwema, bado inaendelea kusambazwa na watu wengi wamevutiwa na kazi yao hiyo kutikana na umahiri wao katka uimbaji na uchezaji, na mpaka sasa wa matoleo 5.
1- Yesu Ni Mwema
2- Zawadi ya Krissmas
3- Naitamani Mbingu
4- Mama Yetu
5- Nakushukuru Mungu
 
Usikose kufurahia kazi yao.
 
By Audax Mathias
AFISA UTAMADUNI
Next Post Previous Post
Bukobawadau