HALI YA MAANDAMANO YA WAISLAAM JIJINI DAR HII LEO
Walioweza kupenya hadi maeneo ya Ikulu hali ilikua hivi
Nguvu iliyotumika kupambana na waandamanaji maeneo ya kariakoo hii leo
Wakati
Zanzibar Sakata la Waislamu kuendeleza kitimtim kufuatia kutoonekana
kwa Kiongozi wa Kundi la Uamsho Vurugu zimeendelea kutawala eneo la
Darajani na kusababisha Polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi
kutawanya watu.
Jijini
Dar es Salaam hali si tofauti na hiyo maeneo ya Kariakoo maduka kadhaa
yamefungwa kufuatia vurugu kama hizo baada ya Swala ya Ijumaa kufuatia
pia kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania
Sheikh Ponda yamekuwa ni matokeo ya vurugu watu kukimbizana huku Polisi
wakidhibiti Usalama na Amani kuelekea harijojo.(Picha na Maktaba).
Maeneo
ya Posta karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani Askari wameweka utepe wa
kudhibiti watu kuingia katika maeneo hayo kitendo kilichosababisha
shughuli nyingi kusimama.
Waandamanaji wakichezea kichapo kikali
Aina yai nVipeperushi vilivyotolewa na Waumini wa Dini ya Kiislamu kabla ya maandamano leo.
Maeneo ya Kariakoo magari ya jeshi JWTZ zaidi ya 8 yakiwa katika doria.