HUU NDIO MKASA ULIOTUFIKIA HII LEO 3/11/2012 !!!
BUKOBAWADAU
3 Nov, 2012
Mdada
aliyekuwa anaishi na jamaa kinyemela alimng'ang'ania jamaa akidai
keshapotezewa sana muda lazima jamaa amuoe. Kila ujanja jamaa aliofanya
mdada kakaza kamba lazima aolewe tu!.Jamaa akaskuti, akapata jibu. Akaingia
facebook kachagua picha za wadada wanne akaziprint, kisha kwenye kila
picha akaandika RIP, akaficha kwenye kitabu akakiweka juu ya TV nyumbani kwake . Mdada
wakati wa kupukuta vumbi akazikuta zile picha akaziangalia akabaki na
maswali kichwani mwake. Jioni jamaa aliporudi swali la kwanza likaanza;
MDADA: Samahani nimezikuta picha za wanawake kwenye kitabu ni akina nani?
JAMAA: Achana na zile picha
MDADA: Zinanishangaza kuna nini?
JAMAA: Niwe mkweli hebu leta hizo picha, huyu wa kwanza anaitwa Jeni,
nilitaka kumuoa wiki mbili kabla ya harusi akagongwa na daladala, huyu
mwingine Sara tulikutana kwenye pati ya kazini tukapanda siku ya
kupeleka posa kwao majambazi wakaingia kwao na kuuwa watu wawili yeye
akiwa moja wapo. Huyu Davidina, alikuwa ndio kwanza katoka kusoma Ulaya
shangazi yangu akanitambulisha tukapendana sana, wajomba wakapeleka posa
kwao wakakuta msiba, aliangukiwa na ukuta wa nyumba iliyokuwa inajengwa
akafa, huyu wa mwisho Esther ndie aliyekuwa mpenzi wangu wa mwisho
kabla ya wewe, tulikuwa karibu tufunge ndoa baba yake akampa pesa aende
Dubai, ndege yao ikaangukia baharini mwili wake haujaonekana, nilikaa
kitambo nikitafakari hii mikosi kabla ya kuoa lakini nimeona ilikuwa
bahati mbaya tu, ndio tukaonana na wewe. Na kiukweli nimeamua lazima
nipeleke posa kwenu kesho.
MDADA: Posa sawa hata mimi nataka
ulete, lakini ungengoja kwanza kesho asubuhi ntaenda kuwaona wazazi,
unajua sijawaona muda mrefu, nikae huko kidogo halafu ntakubonyeza lini
ulete posa
JAMAA: Sawa lakini usichelewe sana
MDADA: Zinanishangaza kuna nini?
JAMAA: Niwe mkweli hebu leta hizo picha, huyu wa kwanza anaitwa Jeni, nilitaka kumuoa wiki mbili kabla ya harusi akagongwa na daladala, huyu mwingine Sara tulikutana kwenye pati ya kazini tukapanda siku ya kupeleka posa kwao majambazi wakaingia kwao na kuuwa watu wawili yeye akiwa moja wapo. Huyu Davidina, alikuwa ndio kwanza katoka kusoma Ulaya shangazi yangu akanitambulisha tukapendana sana, wajomba wakapeleka posa kwao wakakuta msiba, aliangukiwa na ukuta wa nyumba iliyokuwa inajengwa akafa, huyu wa mwisho Esther ndie aliyekuwa mpenzi wangu wa mwisho kabla ya wewe, tulikuwa karibu tufunge ndoa baba yake akampa pesa aende Dubai, ndege yao ikaangukia baharini mwili wake haujaonekana, nilikaa kitambo nikitafakari hii mikosi kabla ya kuoa lakini nimeona ilikuwa bahati mbaya tu, ndio tukaonana na wewe. Na kiukweli nimeamua lazima nipeleke posa kwenu kesho.
MDADA: Posa sawa hata mimi nataka ulete, lakini ungengoja kwanza kesho asubuhi ntaenda kuwaona wazazi, unajua sijawaona muda mrefu, nikae huko kidogo halafu ntakubonyeza lini ulete posa
JAMAA: Sawa lakini usichelewe sana
BUKOBAWADAU
Bukoba Wadau ni mtandao unao toa habari na matukio yanayo tokea katika mji wa bukoba pamoja na mkoa wa kagera kwa ujumla.
Email:bukobawadau@gmail.com | Phone :Mc baraka:0784 505045, 0754 505043
Instagram @bukobawadau | Facebook @bukobawadau