Bukobawadau

MAMIA WAJITOKEZA KATIKA SHUGHULI YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU DEUSDEDITUS R.RWABIZI

Mjane wa Marehemu Deusdeditus akiangua kilio kikubwa wakati wa kuaga mwili wa marehemu Mumewe muda mchache kabla ya kuanza safari ya kuelekea kijijini kwao Buganguzi yatakapofanyika Mazishi.
Tukio lililovuta hisia za watu wange wakati Mjane wa Marehemu na mwanae mmoja wakiangua kilio  wakati wa shughuli ya kuaga Mwili wa Marehemu iliyofanyika katika Hospital ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam kabla haujasafirishwa mwili wake kupelekwa Kijijini kwao Buganguzi Muleba Kagera yatakapofanyika mazishi kwa siku ya Ijumaa.
 Mjane wa marehemu akisaidiwa baada kushindwa kuvumilia aliposhuhudia mwili wa marehemu mumewe
 Mjane wa Marehemu akibusu kwa uchungu mwili wa mmewe Marehemu Deusdeditus Rwabizi.
 Mmoja wa Ndg wa Marehemu Deusdeditus Rwabizi akitoa machozi katika kuaga mwili wa Mdogo wake.
Heshima ya mwisho wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Deusdeditus Rwabizi
Mazishi ya Marehemu yatafanyika nyumbani kwao Kijiji cha Katare Kata ya Buganguzi wilaya ya Muleba Mkoani Kagera.
 Ni uzuni mkubwa kwa ndugu na jamaa wa familia ya Marehemu Deusdeditus M.Rwabizi ni kufuatia kifu chake baada ya kukutwa amejinyongonga Numbani kwake Chumbani.
 Wadau wakiendelea kushuhudia mwili wa Marehemu
Bi Florida Muhazi mmoja wa wadau walioudhulia
 Mdau Grace Muhazi.
 Mdau Ben Mulokozi akitoa mkono wa pole kwa Ndugu wa familia ya Rwabizi.
Mmoja wa rafiki wa Marehemu aishuhudia.
 Anaonekana Mdau Titus Bushaija (katikati ambaye ni msemaji wa familia yaRwabizi  na mwenyekiti wa shughuli hii akipokea pole.
Wadau waliofika kuaga mwili wa Marehemu.
Mdau Delfinius Penessis kushoto, Mzee Tibaigana (katikati)na Mzee Isaack ni sehemu ya wadau walioudhulia
 Sehemu ya vijana kutoka pande za Buganguzi  wakionyesho ushirikiano mkubwa katika tukio hili.kutoka kushoto Mdau Mwambi, Florence, Mdau Gody na OMG Alex Tibaigana

 Taswira ya wadau waliojitokeza katika shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Deusdedtus. R.Rwabizi.

Katikati ni Mjane wa Marehemu na mwanae pekee wa kiume.
 Sehemu ya mashuhuda waliojitokeza kuaga mwili wa Marehemu
BUKOBAWADAU BLOG TUNATOA POLE KWA NDUGU NA JAMAA WOTE WALIOFIKWA NA MSIBA HUU.

MATUKIO ZAIDI GONGA NENO OLDER POST
Next Post Previous Post
Bukobawadau