Bukobawadau

MATOKEO YA FORM FOUR YATANGAZWA.


 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa (Mb) akimuelekeza jambo Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo. Mh Philipo Augustino Mulugo kabla ya kuanza kutangaza matokeo ya kidato cha nne mbele ya baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali, kwenye makao makuu ya ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam

SERIKALI imetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 ambapo kwa mwaka huu idadi ya wanafunzi waliofeli imeongezeka na kufikia laki mbili na arobaini.

Mbali na ongozeko la idadi ya wanafunzi waliofeli , ufaulu wa wanafunzi wa kike umekuwa mdogo ukilinganishwa na wa kiume.

Kati ya watahiniwa 126,847 ni watahiniwa 397,136 ndiyo waliofanya mtihani huo, wasichana waliofaulu ni 46,181 wakati wavulana waliofaulu ni 80,686 huku Waliofutiwa mtihani ni 789 kwa kosa la kuandika matusi katika mitihiani yao.

Shule kumi zilizotajwa kufanya vizuri ni pamoja na st. francis ya mkoani mbeya, marian wavulani ya pwani na fedha wavulana ya dar eslsaama.
gonga hapa kuingia

KUPATA MATOKEO BOFYA HAPA;http://www.matokeo.necta.go.tz ama pitia kwenye blog marafiki pembeni kulia mwa blog.




    Next Post Previous Post
    Bukobawadau