Bukobawadau

SHULE YA WASICHANA YA SEKONDARI YA RUTH MSAFIRI

Na, Judith Blasio

Shule kukabidhiwa kwa wananchi ni vita na viini macho vya kisiasa.
Adhaniaye amesimama na angalia sana asi.....................
Oh nampa pole sana  mh mbunge aliyemaliza muda wake na kumfariji kuwa uwe mpole sana katika hili na usikwazwe. Wewe hi mwanamaombi liombee hili na songa mbele utauona mkono wa bwana.
Wananchi wa katoke nawapeni pole kwa kutwishwa mzigo na wachache wenu wanadiriki kutumia kivuli cha jamii kutenda unyama bila aibu wala woga. Kiumbe usimwogope binadamu lakini mwogope Mungu.

Cha mno chunga sana jasho la mtu binafsi likienda bwelele bila hata hata ahsante -wapendwa wazalendo wanakijiji hapo hakuna baraka kabisa.
Mwalimu mwenzagu mheshimiwa mkuu ngoma ilinoga lakini fuatilia sana kwa kina ukweli haujajua na tafadhali ukiujua ukweli usione aibu kutueleza.
Kaka yangu mh diwani wa katoke wewe wajua kilicho ndani ya moyo wako pengine utatuzi usio na washangiliaji ungefaa zaidi kwani wacheza ngoma wanacheza mlio wa ngoma bila kujua kilicho ndani ya ngoma.
Bukoba wadau mimi hayo ndio machache yangu kama mwana kijiji na ndugu wa damu.

Na,Judith Blasio 
judblasio@yahoo.co.uk
Next Post Previous Post
Bukobawadau