USIKU WA VALENTINE BUKOBA,WALKGARD ANNEX KWALIPUKA SHANGWE ILE MBAYA!!
Taswira ya kaunta ndani ya Walkgard Annex Hotel.
Mkurugenzi wa Walkgard Annex mama Adventina Matungwa akifungua rasmi shughuli hii.Mama huyu anakua mfano wa ni vipi mtu utoke kwa siku kama hii,kwa upendo mkubwa mama huyu ananing'ata sikio kuwa asilimia 20 ya mapato ya siku hii(yaani faida yake) anawapa kituo cha Radio cha Kasibante wakiwakilishe kwa watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu.
Mzee Mchuluza akishow love na familia yake.
Mdau Alley Simba na mkewe na mdada ambaye ni mgeni machoni mwetu,ila shughuli yake daahh!!
Hivi ndivyo ilivyo wakirisha familia ya Ndg Mganyizi Zachwa.
Wanaonekana wanadada pichani kutoka kushote Bi Salome chui na London,Bi Lilian Peter Mwise na Bi Maua Ramadhani.
Mr na Mrs Patrick pombe walikuwepo.
Hakika watu wameweza kuitikia.
Kwa mtambo akiwa amesimama Dj Mkongwe katika tasnia hii ya burudani, na upande wa Mc's mshereheshaji wa shughuli hii Bi Joyce Lubozi pichani (kushoto)alihusika na kumudu vyema.
Watu walivyo enea vyema ukumbini.
Mdau Fide akiwakilisha kwa mbwembwe upendo wake ila kubwa zaidi ni vile alivyoichukulia siku hii kaipa heshima yake kwa kuwa smart ile mbaya na utulivu mkubwa
Mr & Mrs Deo Rugaibura,kaka yetu huyu na familia yake ni mfano wa kuigwa,jamaa anaishi kama yupo majuu,upendo na pia anajuwa kupangilia vitu,walipendeza sana hawa wadau,BIG UP KAKA DEO
Meza ya familia ya Mama Muhazi,Mama yetu huyu anastahili tuzo ya heshima maana naye ni mfano wa kuigwa,ni mama mpambanaji hasa,mengi zaidi nitafute pembeni,HESHIMA YAKO MAMA
Kushoto ni mwanadada Devotha kama ilivyo kawaida kutunisha mambo flani, pembeni ni Mwanadada jina kapuni kwa maelekezo tuliyopewa.
Kama hawa ndio walikuwa sehemu ya walengwa,eeeh maana kujizeesha na kujiweka nyumbani mwaka hadi mwaka sio mambo,asante sana Mzee wetu Stanford na familia yako kwa kuunga mkono juhudi za waandaaji
Kutoka na familia ndilo jambo tunahimiza sana pale nafasi inapokuwepo,asante Mzee Mushobozi
Jopo likiendelea na mchakato wa kutafuta washindi kwa usiku huu.
Burudani ikiendelea chini ya Dj Max
Wadada hawa pia ni muhimu sana katika jamii maana ni wa kileo wasio na zengwe na mtu yoyote,wanadai raha jipe mwenyewe ikibidi,safi sana dada Rehema,Devota na bi Maua Ramadhani
Burudani imeshika kasi,namuona Super Mkude akisakata na mwanae Mainda pembeni Jumanne Bingwa,Mrs Mohamed Kassim kwa mbali Mrs Mkude wakionesha furaha sana kwa kucheza muziki.
Watu wakishow love ni changanikeni wanaume, wanawake, wapenzi mle mle,kaka, dada,baba, na mama zao
Furaha yote hii inaletwa kwako na www.bukobawadau.blogspot.com.
Hapa ninachoweza kusema ni kwamba Wamjini utawajua tu!!
Wana wa kikwemu pichani anaonekana Bi Jamila na Bi Zena.
Mdau Jamal Kalumuna na familia yake,Big up sana Jamco.

Hapo ni washindi kwa shindano la wale wa miaka 35 mpaka 45 nao ni Mrs Agneta Kalike na Mrs Gode Bayona,hakika walikuwa wamewaka na mchakato wa kupata washindi ulikuwa wa uhuru na haki kabisa,savuu kwenu wanamama.
Zawadi ya mwisho ilikuwa ya shindano kwa wenye miaka 45 na kuendelea,ndipo meneja wetu Mr Mushobozi na mke wake wakaibuka washindi,hakika walikuwa kifamilia zaidi pozi zao,umakini na kupendeza viliwapa ushindi,pichani wakipokea zawadi kutoka kwa Afisa utamaduni Mr.Rugeiyamu
Ushindi ni raha jamani,hapo washindi wameungana na watoto wao kupata picha ya pamoja na wazazi wao, kwa msisitizo zaidi WALKGARD wametoa zawadi pia na CHETI kwa washindi na kusema ni vyema ukitunze maana ni sehemu ya CV zakooooo aaaaah aaaah aaaaah huwezi kujuwa kuna leo na kesho
Taswira kuelekea ukumbini
Mama Mick akibadilishana mawazo na mdau mwenzake
Shuguli ni watu kula kunywa na kufurahi
Mdau Muhamed Kassim naye ndani.
Mwanadada Lilian Peter.
BUKOBAWADAU TUMEFURAHISHWA SANA NA SHUGHULI HII TANGU ZOEZI ZIMA LIMEANZA MPAKA MWISHO ATUKUAMINI NAMNA WATU WALIVYOKUWA WANANUNUA MEZA KABLA YA SIKU NA WALIVYOJITOKEZA KWA WINGI HUKU WAKIWA WAMEPENDEZA KWA KUTUPIA/KUNYUKA PAMBA KALI!!!
Mzee Sadi Idd na Mdau Top mzee wa balo.
Mdau kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho, huu ndio mwisho wa taswira ndani ya WALKGARD ANNEX kwa usiku wa wapendanao,baada ya hapo libeneke letu likaendelea ndani ya kisima ndani cha burudani ndani ya Club linaz matukio ya zaidi utayapata kupitia facebook page yetu.
Mzee Sadi Idd na Mdau Top mzee wa balo.
Mdau kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho, huu ndio mwisho wa taswira ndani ya WALKGARD ANNEX kwa usiku wa wapendanao,baada ya hapo libeneke letu likaendelea ndani ya kisima ndani cha burudani ndani ya Club linaz matukio ya zaidi utayapata kupitia facebook page yetu.